DC Hai,awataka wafanyakazi kufanya kazi kwa ubunifu ,kama serikali inavyo hitaji kutumikia wananchi wake.



 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai Yohana Sintoo(kushoto),Mkuu wa Wilaya ya Hai Gelasius Gasper Byakanwa(katikati) na Katibu Tawala wa Wilaya ya Hai Upendo Wela,wakifuatilia uwasilishwaji wa  wa taarifa za ubunifu katika idara.


Afisa Elimu Msingi Agnes Luhavi akielezea Ubunifu ulio fanywa katika idara yao,katika shindano la Ubunifu lililo anzishwa na Mkuu wa wilaya ya Hai.


Wafanyakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai wakifuatilia uwasilishwaji wa ubunifu katika idara zilizo kuwa zikishindanishwa

Wafanyakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai wakifuatilia uwasilishwaji wa ubunifu katika idara zilizo kuwa zikishindanishwa

Hai-Kilimanjaro.

MKUU wa wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro Gelasius Byakanwa amezitaka idara zote za Halmashauri ya wilaya ya Hai kuhakikisha kuwa  wana kuwa wabunifu kiutendaji ili kuweza kuhudumia jamii katika ubora unao hitajika na serikali.
Ameyasema hayo jana wakatika wa muendelezo wa  shindano  alilo lianzisha la utoaji wa tuzo kwa idara inayo fanya vizuri kila mwisho wa mwezi ili kuweza kuonesha ufanisi wa kazi zao kwa jamii wanayo ihudumia.
“Nipende kuwa weka wazi kuwa kila idara inapaswa kushiriki kikamilifu katika shindano hili ili kuweza kuacha kufanya  kazi kwa mazoe ya kukaa ofisini na  kusubiri taarifa toka nje,badala yake fanyeni kazi kwa kuifikia jamii ili kuweza kudhibiti ukiukwaji unao weza kufanywa na watu mapema,na kwa kufanya hivyo itakuwa ni rahisi katika utendaji wa idara husika.”alisema Byakanwa.
Katika mashindano hayo yaliyo shirikisha idara tatu ikiwemo idara ya  Elimu Msingi,Idara ya Elimu Sekondari na Idara ya ujenzi na zima moto,washindi waliweza kupatikana ambapo idara ya Ujenzi na zima  moto iliweza kuibuka mshindi na kukabidhiwa Kikombe cha ushindi.
Kwa upande wake wa Mkandarasi toka Idara ya Ujenzi na zima moto Philipians Msangi ameeleza kuwa jitihada za ubunifu zinazo fanywa na idara hiyo zimeweza kuzaa matunda na kukubalika na wataalamu wengine ,ikiwa ni pamoja na kufanya kazi zilizo shindikana kufanywa na wazabuni wa nje  kutokana na kiasi cha fedha kuwa kikubwa.

“Ukiangalia wazabuni wa njee wanaopewa kazi mara nyingi wameonekana kushindwa kukamilisha kwa wakati au kutumia fedha nyingi nabado kazi isionekane ila sisi tumeweza kufanya na kuisidia Halmashauri yetu kupiga hatua.Alisema Msangi.