DED HAI:WANAO JIONA KUWA NI MAPAPA WA KUHUJUMU RASILIMALI MAJI WASIFUMBIWE MACHO.


Mkurugenzi wa Halimashauri ya Wilaya ya Hai Yohana Sintoo,akisifu ubora wa mazingira katika bodi ya maji Losaa Kia katika chanzo cha maji Ulengu kilichopo Kata ya Masama Mashariki.

Mkurugenzi wa Halimashauri ya Wilaya ya Hai Yohana Sintoo,akipanda mti aina ya Mti karanga katika bodi ya maji Losaa Kia katika chanzo cha maji Ulengu kilichopo Kata ya Masama Mashariki.

Afisa misitu kata ya Masama Mashariki John Katikiro akipanda mti katika bodi ya maji Losaa Kia katika chanzo cha maji Ulengu kilichopo Kata ya Masama Mashariki.


Mtambo unao tumika kuweka kiwango cha dawa ya kutibu maji katika bodi ya maji Losaa Kia katika chanzo cha maji Ulengu kilichopo Kata ya Masama Mashariki.

Mhasibu wa  bodi ya maji Losaa Kia Senyaeli Nko akisoma risala katika bodi ya maji Losaa Kia katika chanzo cha maji Ulengu kilichopo Kata ya Masama Mashariki.



Mafundi bomba wanaotumika kufanya kazi katika bodi ya maji Losaa Kia katika chanzo cha maji Ulengu kilichopo Kata ya Masama Mashariki,wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Halimashauri ya Wilaya ya Hai akitoa maelekezo.


Hai-Kilimanajro
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Hai ndugu Yohana Sintoo  ameipongeza bodi  ya maji Losaa Kia kwa utunzaji bora wa mazingira huku pia akiahidi kutumia sheria za maji katika kulinda rasilimali maji ambayo ni muhimu kwa uhai wa binadamu.

Sintoo ameyasema hayo hii leo katika chanzo cha maji cha Ulengu ikiwa ni mwendelezo wa wiki ya maji ambapo amesema kuwa ili kutatua changamoto zilizopo ni vyema sheria zikafuatwa pasipo kumuogopa mtu yeyote.

Sanjari na hayo mkurugenzi ameagiza uongozi wa bodi hiyo ya maji kufuatilia madeni kwa wateja sugu ikiwa ni njia ya kuzikabili changamoto zilizopo ambapo pia kupitia madeni hayo yatasaidia kupanua miundo mbinu ya maji.

“Niagize bodi za maji kuhakikisha kuwa wana kusanya madeni yote yalio nje kwa wateja ambao ni wadaiwa sugu,ambao wamekuwa mapapa,wakidaiwa kila siku pasipo kulipa,msiwafumbie macho wachukulieni hatua za kisheria maana hao ni wahujumu maji”alisema Sintoo.

Moja ya changamoto kubwa inayoikabili bodi hiyo ya Losaa Kia ni pamoja na ongezeko la watu ambapo awali mradi huo ulitegemewa kuhudumia watu wasiozidi elfu sitini na sasa mradi huo unahudumia watu zaidi ya elfu sabini.

Kwa upande wake Mhasibu wa bodi ya maji Losaa Kia Senyaeli Nko kwa niaba ya Mwenyekiti wa bodi ya maji wilaya Epafra Urassa amesema kuwa bodi hiyo ya maji imekuwa ikikabiliwa na changamoto lukuki ikiwemo uharibifu wa mazingira unao fanywa na binadamu ikiwemo kulima katika vyanzo vya mito na chemichemi ,kukata miti rafiki kwa mazingira pamoja na kuharibu miundombinu ya maji jambo linalo pelekea maji kupungua.

“Tunasikitika kuona kuwa uharibifu huu unafanywa na wananchi ambao wanayo elimu ya umuhimu wa utunzaji wa mazingira,nah ii ni hatari kwa usambazaji wa maji kwani kiwango kilicho kusudiwa kupelekwa kwa wananchi kinapungua.”Alisema Nko.


Wiki ya maji inaendela na inatarajika kukamilika wiki hii ambapo maadhimisho yake katika mkoa wa Kilimanjaro  yatafanyika hapa wilayani Hai huku wiki ya maji ikienziwa kwa upandaji miti katika vyanzo vya maji na kauli mbiu ikiwa ni “PANDA MITI KUTUNZA VYANZO VYA MAJI”.

Picha na Haikaziblog.