WAKULIMA WILAYANI HAI WATAKIWA KUJIPANGA NA KILIMO CHENYE FAIDA CHA ZAO LA MACADAMIAS (KARANGA MTI)


Mkuu wa Wilaya ya Hai Gelasius Byakanwa wa kwanza upande wa ( kulia) akipata maelekezo ya njia ya kupandikiza mmea huo(Macadamias) toka kwa mwekezaji wa shamba hilo la Mbosho Coffee,James Paul.





Mkuu wa Wilaya hiyo Gelasius Byakanwa pamoja na Katibu Tawala Wilaya Upendo Wella,wakisoma maelezo ya nafaka ya Academia mara baada ya kupakiwa katika mifuko tayari kwa matumizi.
Pichani ni zao la Macadamias (karanga mti) mara baada ya kuvunwa tayari kwa maandalizi ya kuikoboa na kupata kiini cha ndani ambacho ndicho kinacho hitajika.

Hai-Kilimanjaro.

Wananchi Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro,wameshauriwa kuanza kulima zao la biashara aina ya Macadamias  alimaharufu kama karanga mti ili kuweza kuongeza kipato chao,kutokana na zao hilo kuwa na uhitaji mkubwa katika masoko ya ndani na nje ya nchi .
Rai hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Wilaya ya Hai Gelasius Gasper Byakanwa wakati alipotembelea shamba la Mbosho Coffee linalo milikiwa na muekezaji James paul,kwa lengo la kupata ufafanuzi wa zao hilo la biashara ili kuweka utaratibu wa wananchi kushauriwa kulima zao hilo.
Amesema kuwa kutokana na Mwekezaji huyo kuanza kuzalisha zao hilo ambalo linahitajika sana kwa masoko ya nje,kutokutosheleza lengo la wateja,ni vema wananchi kujipanga kulima zao hilo pindi taratibu zitakapo kamilika sambamba na ushauri toka kwa wataalamu wa kilimo wilaya.
“Nimevutiwa sana na muwekezaji huyu kwa zao lake hili,vilevile nimependezwa na mpango wake wa kutaka kuwashirikisha wananchi kulima zao hili ili watu  weyu wapate faida”alisema Byakanwa.
Byakanwa ameongeza kuwa,mara baada ya kumalizika ushirikishwaji kwa pande zote zinazo husika katika masuala ya kilimo,wananchi watapata fursa ya kupewa elimu ili kuanza zao hilo lenye kipato kikubwa mara moja.
Kwa upande wake mwekezaji huyo James Paul,amemshukuru Mkuu wa Wilaya  kwa kutembelea shamba hilo ikiwa ni pamoja na kusikiliza baadhi ya changamoto zinazo mkabili ikiwemo uharibifu wa zao hilo toka kwa Wanafunzi wa shule ya sekondari Mbosho.
Amesema kuwa ikiwa serikali itapendekeza zao hilo kulimwa kwa wingi,yupo tayari kutoa miche ya zao hilo ili wakulima waweze kuipata na kufaidi biashara yake iliyo na fedha nyingi.

“Tusipende kufanya kazi rahisi rahisi za kupata faida kwa haraka,ila tujenge utamaduni wa kuwekeza kwa muda mrefu na kupata faida kwa muda mrefu kupitia zao hili,ambapo kila familia na kizazi kijacho kita nufaika na zao hilo”alisema Paul.