MADIWANI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA HAI WAMSIFU MKUU WA WILAYA NA MKURUGENZI KWA KUWAWEKA PAMOJA.


Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai,(katikati) ni Mkuu wa Wilaya ya Hai Gelasius Byakanwa na wa mwisho (kulia) ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai.
HAI-KILIMANJARO

Mkuu wa wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro Gelasius Gasper Byakanwa amewataka Madiwani katika Halmashauri ya Wilaya ya hiyo kufanya kazi kwa Uangalifu na kwakushirikiana ili kuleta maendeleo wilayani hapo.

Ameyasema hayo katika ufunguzi wa semina ya siku mbili kwa madiwani wa halmashauri ya wilaya iliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya Ya Hai ambapo amewataka Madiwani kuwa vipaumbele na kuhakikisha miradi inayoanzishwa kwenye jamii iwe imenzishwa na wananchi wenyewe ili kuiwezesha jamii kuwa na uwezo wakujitegemea kwaajili ya maendeleo yao.

Byakanwa ameongeza kuwa maendeleo katika jamii hayangalii itikadi za chama hvyo ni wajibu kwakila kiongozi hususa ni madiwani hao kushurikiana na jamii kuainisha miradi ambayo tayari imefikia hatua inayostaili kupewa fedha, na kusisitiza kupewa taarifa ya mtu yoyote ambae anakwamisha  miradi hiyo bila kumuonea mtu wala kujali kuwa anatoka chama gani.


Nae mwenyewkiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai Bi.Helga Mchovu amemshukuru mkuu wa Wilaya kwa juhudi zake za kushirikiana na Madiwani hao katika mambo mbalimbali hususa kuleta maendeleo kwa wananchi na Halmashauri kwa ujumla,huku akiwataka madiwani kufanya kazi na kushirikiana na wananchi katika kuleta maendeleo katika jamii.

"Nipende kukupongeza Mkuu Wetu wa Wilaya pamoja na Mkurugenzi kwa kazi nzuri munazo fanya ikiwa ni pamoja na njia munazo fanya ya kushirikiana na sisi Madiwani katika nafasi ya kuleta maendeleo kwa wilaya yetu,nafurahi kwakuwa hatuna uchama katika shughuli za maendeleo"alisema Mchomvu.