MWEKEZAJI WA KIWANDA CHA AFRICAN VEGETABLES WILAYANI HAI,ATAKIWA KUTHIBITISHA KUWA CHINI YA EPZA.

Kiwanda cha African Vegetables kilichopo Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro.
HAI-KILIMANJARO

Mwekezaji wa kiwanda cha African Vegetables kilichopo Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro Andry Emmanuel,ametakiwa kutoa uthibitisho wa uwekezaji wake kuwa chini ya EPZA,kutokana na kuonekana kuwa hauja kidhi vigezo vinavyo takiwa na EPZA.

Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Hai Gelasius Gasper Byakanwa wakati alipo tembelea bodi ya shamba la  Nshara Amcos saccos katika eneo la Makuru Estate linalo simamiwa na chama hicho.

Amesema kuwa mwekezaji huyo kulipa kodi isiyo endana na uwekezaji wake huku akiwa amefutiwa kodi ni jambo lisilo kubalika  na serikali kutokana na mapato ya serikali kupotea bila sababu ya msingi.

“kwa kuonesha kuwa yupo chini ya EPZA na kulipa kodi ya shilingi laki saba na sitini na tano jambo hili siyo sawa tena ukizingatia ni kwa ukubwa wa eneo la ekari 471,Kumuita mwekezaji anafaaa kuitwa hivyo laikini siyo kwa daraja la EPZA,kama analipa kodi ya kuanzia milioni hamsini na kuendelea,angalau serikali ingekuwa inapata hizo pesa ange kubaliwa kuwa chini ya EPZA”alisema Byakanwa.

Byakanwa alitoa ufafanuzi kuwa wawekezaji walio chini ya EPZA wanapaswa kuhakikisha kuwa wameajiri idadi ya watu wengi ambao wanaweza kupata ujuzi na maarifa kipindi chote wawapo kazini,kampuni kuwa na uwezo wa kuzalisha kuanzia tani nne na kuendelea ambapo serikali ndipo huwa futia kodi kwa miaka kumi kutokana na mchango wao kuonekana na kutambulika.

“Inashangaza kuona  kuwa kampuni hii ipo chini ya EPZA lakini uzalishaji wake ni mdogo kwani wanauwezo wa kuzalisha tani moja na huku idadi ya wafanyakazi wakiwa hamsini,pasipo wafanyakazi hao kuto kupata ujuzi kama EPZA inavyo taka,kwani kazi waliyo nayo ni kuchemsha maharage wanayo zalisha katika kampuni hiyo tu”.

Katika hatua hiyo Mkuu huyo wa Wilaya alimtaka mwekezaji huyo kufika ofisini kwake kabla ya tarehe 2 mei mwaka huu mara baada ya mwekezaji huyo kurudi toka safarini, akiwa na vigezo na viambatanisho vinavyo muonesha kuwa yupo chini ya EPZA kihalali.

Kwa mujibu wa maelezo ya Meneja wa Kampuni hiyo Rudy Asukile amesema kuwa uzalishaji wa kampuni hiyo hauja fikia kiwango cha kuwa chini ya EPZA kama inavyo takiwa kutokana na uzalishaji kuwa mdogo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Nshara Amcos Saccos Abick Uronu amesema kuwa, kwa kipindi cha mwaka 2016-2017 mwekezaji huyo anadaiwa kiasi cha shilingi milioni 81 ambazo alipaswa kulipa toka Julai 1. 2016,jambo linalo pelekea kukwamisha shughuli na utekelezaji wa miradi ya jamii na chama  kama ilivyo kusudiwa.

Kampuni hiyo inahusika na usindikaji wa maharage mabichi ambayo husafirishwa nje ya nchi kipindi chote cha uzalishaji wa nafaka hiyo.