HAI-KILIMANJARO
Mkurugenzi Mtendaji
wa Halmashauri ya wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro Yohana Sintoo amewataka
walewote walio bainika kuwa na vyeti feki kuhakikisha wanafuata maagizo yaliyo
tolewa na Rais kwa kuachia nafasi zao kabla ya mei 15 mwaka huu .
Akizungumza
na wanachama wa chama cha wafanyakazi (TWALGU) Wilaya ya Hai mara baada ya maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani
Mkurugenzi huyo,amewataka wafanyakazi hao walio bainika kuwa na vyeti feki kuanza
kujipanga kufanya kazi nyingine ili kuweza kupunguza ukali wa maisha kwa
kufanya kazi ambazo hawakutegemea.
Amesema kuwa
wafanyakazi hao wanatakiwa kufuata maelekezo ya kiserikali yaliyo tolewa ili
kuweza kuepuka usumbufu utakao jitokeza kwa kukaidi maagizo yaliyo tolewa ya
kuwataka kusimama kufanya kazi.
“Niwaambie
kuwa huu siyo mwisho wa kufanya kazi ya kujitafutia kipato na kuiangalia
familia,zipo kazi nyingi za ujasiriamali za kufanya,naamini kuwa wafanyakazi
hao walisha pata semina mbalimbali za ujasiriamali zitakazo wasaidia”alisema
Sintoo.
Katika taarifa
ya watu wenye vyeti feki iliyo tangazwa na raisi
kuizungumzia hivi karibuni watu 19,706 wamebainika,ambapo kwa mwezi
Taifa limekuwa likipoteza bilioni 19 na milioni 848, na mwaka mzima Taifa limekuwa
likipoteza kiasi cha shilingi bilioni 230 kwa kuwalipa mshahara watu wenye
vyeti feki.
Wafanyakazi walio
bainika kuwa na vyeti feki wilaya ya Hai
ni takribani wafanyakazi 74 kutoka idara na vitengo mbalimbali.