DED HAI:WACHUNGAJI MSITEGEMEE KAPU LA SADAKA ZINAZO TOLEWA NA WAUMINI WENU FANYENI KAZI.


Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai  Yohana Sintoo,akitoa somo kwa Wachungaji na Wake zao wa Makanisa ya Kipentekoste,awataka wafanye kazi wasitegemee kikapu cha sadaka.


HAI-KILIMANJARO.
VIONGOZI wa madhehebu ya dini wametakiwa kufanya kazi kwa bidii ili kujiongezea kipato na kuacha  tabia ya kutegemea sadaka zinazotolewa  na waumini  kuendeshea maisha yao

Wito huo umetolewa na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya Hai mkoani Kilimanjaro , Yohana Sintoo wakati akizungumza na viongozi wa Bazara la makanisa ya Kipentekoste mkoani hapa (C.P.C.T) walipokutana katika kanisa na T.A.G Elishadai Bomang’ombe

Alisema viongozi wa dini wanatakiwa kuwa mfano mzuri katika kufanya kazi zinazozalisha na kuacha tabia  kutegemea sadaka inayopatikana kwenye makanisa hayo jambo ambalo limechangia kuwepo kwa migogoro ya kidini pindi hali ya mapato inapopungua .

“Viongozi wa dini mnatakiwa kuwa mfano mzuri kwa jamii mnayoiongoza kwa kufanya kazi kwa bidii na kuepukana na kutegemea sadaka pamoja na misaada  kwa kufanya hivyo mtakuwa mfano mzuri kwenye jamii” alisema Sintoo

''Kuna  baadhi ya viongozi wa dini hawataki kujishughulisha kwa kufanya kazi hata kidogo kazi yao kubwa ni kusubiri sadaka kutoka kwa waumini wao hauipendezi tunatakiwa kufanya kazi ili kupeleka watoto wetu shule''alisema

“Pamoja na kuwatunza watu  kiroho ni lazima tujishughulishe kwa shughuli nyingine za uzalishaji pamoja na kuwaendeleza  watoto wetu kielimu haipendezi kuona mtoto wa mchungaji akiwa anazurura mtaani kwa kukosa ada ya shule ” alisema

“ Tunategemea viongozi wa dini wawe mfano wa kuigwa kwa kufanya matendo mema, kujishughulisha na kuendeleza watoto wao pamoja na kuwafundisha waumini waumini wao namna ya kujikwamua kiuchumi ”
 “ Rais wetu John Pombe Magufuli ameshatoa maelekezo kuwa watu wote wafanye kazi, tena wafanye kazi kwa nguvu zao zote ili kujiongezea kipato kwa familia na Taifa kwa ujumla''alisema Sintoo, 

Alifafanua kuwa  Serikali inatambua mchango mkubwa wa Viongozi wa dini katika kupunguza Imani potofu, na kutatua migogro ndani ya familia na jamii kwa ujumla, hivyo huchangia kupunguza vitendo viovu katika jamii. 

Awali akisoma risala ya  baraza hilo , mchungaji Werande Munis, alisema lengo la kusanyiko hilo ni kufanya ibada ya pamoja na kufahamiana ili kudumisha  ushirika wa watumishi wa Mungu katika wilaya hiyo


Hata hivyo baraza hilo linatoa pongezi za dhati kwa Rais Jamhuri wa Muungano wa Tanzania , John Pombe Magufuli kwa jitihada zake za kufufua uchumi na kutetea maslahi ya Taifa  na watu wake kwa uzalendo na ujasiri.