RC:KILIMANJARO ATINGA SHAMBANI KWA FREEMAN MBOWE KUJIONEA UHARIBIFU WA MAZINGIRA.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira (kushoto) akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Hai Gelasius Byakanwa(kulia) katika shamba la Kilimanjaro Veggies linalo milikiwa na Mbunge wa Hai Freeman Mbowe alipo litembelea.


HAI-KILIMANJARO

SERIKALI mkoani Kilimanjaro imesema kuwa hatua zilizochukuliwa na mkuu wa wilaya ya Hai Gellasius Byakanwa za kuondoa miundombinu ya umwagiliaji  katika shamba la Kilimanjaro Veggie si za kisiasa bali ni taratibu za kisheria za kulinda vyanzo vya maji.

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghira  alitoa kauli hiyo wakati alipotembelea shamba hilo lililopo kijiji cha Nshara ili kujionea hali halisi ya uharibifu wa mazingira   uliofanywa katika eneo hilo linalomikiwa  na mbunge wa jimbo la Hai, Freeman Mbowe.

Alisema hatua zilizochukuliwa na mkuu wa wilaya ya Hai pamoja na mamlaya ya kusimamia mazingira (NEMC)ni hatua sahihi za kulinda vyanzo vya maji pamoja na uoto wa asili kwa mujibu wa sharia ya mazingira ya mwaka 2004 .

Alifafanua kuwa endapo mazingira yatatunzwa vizuri kila kitu kitafanyika kwa ufasaha na kutokutunza mazingira kumechangia kupelekea kuwepo kwa migogoro ya mara kwa mara kutokana na kutegemea sana utunzaji vyanzo vya maji katika kutunza mazingira .

Hata hivyo Mghira  alisisitiza kutokuendelea kwa shughuli zozote za kibinadamu katika shamba hilo kwani mmiliki alikwisha kiri kufanya kosa na kupewa adhabu ya kulipa kiashi cha shilingi milioni 18.

Nae diwani wa kata hiyo, Clement Kwayu alimwomba mkuu wa mkoa kuruhusu kuendelea kwa kilimo hicho katika eneo hilo kwa kimesadia kutoa ajira kwa vijana  zaidi ya 50 na pia eneo hilo ni la asili wameweza kulima zaidi ya miaka 40.

Nae mkaguzi wa mazingira wa baraza la hifadhi na  mazingira Taifa kutoka NEMC,kanda ya kaskazini  Novatus Mushi alisema  uamuzi wa  Mmiliki wa shamba hilo umekiuka  sheria ya mazingira kifungu cha 51 kinachokata mtu yeyote yule kutokufanya shughuli za mazingira ndani ya eneo  la
mita sitini kando ya chanzo cha maji.