WAJANE WANAMCHANGO MKUBWA KUELEKEA TANZANIA YA VIWANDA


Wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai Helga Mchomvu, wapili kutoka kulia aliye valia fulana  nyeupe  ni Mwanaharakati wa haki za binadamu Mese ndosi na Mratibu wa Siku ya Wanawake Wajane wilaya ya Hai,wakiwa katika hosipitali ya Wilaya kutoa zawadi kwa akina Mama wajawazito.


Hai-Kilimanjaro.

Wanaume Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro wametakiwa kuwashirikisha wenza wao katika biashara wanazo endesha pamoja na  kuwa ruhusu kufanya kazi walizo somea au kujiajiri ili kupunguza makali ya maisha pindi mwanaume atakapo fariki na kumuacha mwanamke katika hali ya ujane.

Rai hiyo imetolewa na akina mama wajane wa Wilaya ya Hai wakati wa maadhimisho ya siku ya wajane duniani iliyo wakutanisha wanawake wajane toka maeneo mbalimbalil ya wilaya hiyo wakiongozwa na kauli mbiu ‘WAJANE WANAMCHANGO MKUBWA KUELEKEA TANZANIA YA VIWANDA”.

Kwa upande wake Anande Onesmo Salema ambaye ni mjane amesema kuwa changamoto zinazo wakumba wanawake wajene mara baada ya kufiwa ni pamoja na baadhi ya wanaukoo kuwarithisha kwa wanaume wengine ndani ya ukoo,kunyang’anywa mali zilizo achwa,kufukuzwa  pamoja na kunyang’anywa watoto.

Amesema kuwa kitendo cha kurithisha mwanamke kwa mtu mwingine kimekuwa kikiwaumiza wajane kutokana na kukosa huduma stahiki zilizo kuwa zikitolewa na mume ambapo mrithi amekuwa akishindwa kutoa huduma hizo ipasavyo.

“ni ukweli kuwa mrithi hawezi kutoa msaada wa ukamilifu kwakuwa baadhi ya huduma alizotakiwa kuziotoa kwa mjane huzipeleka kwa mke wake hivyo hali hiyo niya uonevu na unyonyaji zaidi ulio kithiri vijijini.”alisema Salema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Hai Helga Mchomvu amesema kuwa tabia ya baadhi ya wanaume kuwakataza wanawake kufanya kazi au biashara ya kutafuta kipato cha familia ni kitendo kisicho kubalika kwani huleta madhara makubwa wakati mwanaume atafariki kuiacha familia katika wakati mgumu,kwani Mwanamke haja zoea kutafuta.

“inashangaza kwa kweli baadhi ya wanaume kuwa kataza wanawake wao kufanya kazi,unakuta mwanaume amekuwa katili katika suala hilo pasipo kujua kuwa ipo siku anaweza kufariki na kumuacha mke na watoto katika mazingira ya kuwa tegemezi”alisema mchomvu.

Akisoma risala ya wanawake wajane mbele ya Mgeni rasmi Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Yohana Sintoo Mama Shangali amesema kuwa Umoja wa Mataifa unatambua kuwa mamilioni ya wajane ulimwenguni kote wanateseka na matatizo makubwa yanayo sukumwa na jamii wanayo ishi ikiwemo  unyanyasaji wa kingono, umaskini wa kiuchumi ulio kithiri,utapia mlo kwa watoto wao na watoto kukosa elimu bora na malazi.

Ameongeza kkuwa mali ambazo mjane amechuma na mume wake zimekuwa zikichukuliwa kinguvu na ndugu wa mume na kuacha familia nyingi zikiishi katika hali ya ukiwa.

Kwa upande wake Mratibu wa maadhimisho hayo kiwilaya mwanaharakati Mese Ndosi ameiomba serikali kuwasaidia wajane katika masuala ya kisheria pindi wanapo dhulumiwa mali zao ili kuweza kuzirudisha mikononi mwao.

“Tunaiomba serikali itusaidie na iwasaidie wajane kwa kuwapa wanasheria wakati wa kesi zao mahakamani ili waweze kupata haki zao stahiki na kuwafanya kuto kujutia hali ya ujane walio nayo”alisema Ndosi.

Amesema kuwa Siku ya kimataifa ya wajane ilibuniwa mwaka 2005 kupitia usaidizi wa wakfu wa Loomba na kutambuliwa rasmi na Umoja wa Mataifa mnamo mwaka 2010.

 Wakfu wa Loomba ulibuniwa mwaka 1997 na Lord Raj Loomba kama njia ya kumkumba mamake ambaye alibaki mjane akiwa na umri wa miaka 37 eneo la Punjab nchini India.


“Aliongeza kuwa Wakfu huo unalenga kuwaelimisha watoto wa waajane maskini na kuwainua wajane kote duniani. Tangu kubuniwa kwa siku ya wajane duniani mwaka 2005 wakfu huo umewaelimisha maelfu ya watoto wa wajane maskini na kuwasaidia zaidi ya watu 27,000 wa familia zao”aliongeza Ndosi.