Wananchi wa Kijiji cha Mkalama Kitongoji cha Kilima Mswaki wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Wilaya ya Hai Gelasius Byakanwa wakati wa mkutano wa kuelezea majibu ya Tume aliyo unda kuchunguza Migogoro Kijijini hapo.
HAI-KILIMANJARO
MKUU wa Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro Gelasius
Byakanwa ameagiza kukamatwa kwa aliye wahi kuwa Mwenyekiti wa Kijiji cha
Mkalama kata ya Masama rundugai kitongoji
cha Kilima Mswaki Paramenti Nailongwa Mollel kwa kosa la kutumia madaraka yake
vibaya pamoja na kujeruhi wananchi kwa silaha kipindi cha uongozi wake.
Ametoa agizo
hilo leo katika mkutano na wanachi wa kijiji cha Mkalama akiongozana na kamati
ya Ulinzi na usalama Wilaya kwa lengo la kutoa majibu ya tume iliyo undwa mwezi
wa nne mwaka huu kuchunguza tuhuma zilizo kuwa zikimkabili aliye kuwa
mwenyekiti wa kijiji hicho ambaye naye alihudhuria kikao hicho na kuwekwa chini ya ulinzi .
Byakanwa
amesema kuwa katika taarifa alizo pokea toka katika Tume iliyo fika kijijini
hapo imebaini tuhuma hizo ikiwa ni pamoja na wananchi kumlalamikia mtuhumiwa huyo kwa kuwadhalilisha kwa kuwapiga
na kuwajeruhi baadhi yao na kuwasababishia ulemavu wa kudumu,kuchochea vitendo
vya kihalifu kama wizi wa mifugo jambo lililo leta migogoro kijijini hapo
pamoja na kushindwa kukabidhi mali ya kijiji na mipaka yake kwa uongozi ulio
fuata.
“Nimepokea taarifa ya watu waliyo hojiwa na tume yangu
wakiwemo wahanga walio pigwa na Mzee huyu Paramenti na wengine kupigwa
risasi,kuchapwa viboko bila sababu za msingi,na muhusika mwenyewe
alihojiwa.”alisema Byakanwa.
Aidha Mkuu
huyo wa Wilaya ameeleza kutofurahishwa na kauli za mtuhumiwa huyo za kusema
amewaweka viongozi mfukoni hivyo kufanya atakalo, na kusema kuwa
kwa kufanya hivyo ni kuichezea serikali iliyo makini kwa kutaka haki na wajibu
unafuatwa pamoja na haki za binadamu.
Waki ongea
katika Mkutano huo mara baada ya
Mtuhumiwa kukamatwa mmoja wa wananchi hao Amekiri mume wake kupigwa na
mtuhumiwa huyo ikiwa ni pamoja na kumbambikizia kesi isiyo eleweka.
Kwa upande
wake Katarina Joseph amesema kuwa mtuhumiwa huyo amekuwa tishio kijijini hapo
kutokana na kutumia mabavu kutatua changamoto za wananchi huku mume wake
akichapwa na kudhalilishwa mbele yake.
“Mume wangu
aliwahi kupigwa viboko na Mtu huyu kwa kosa lisilo julikana mbele yangu na
watoto wangu kisha kumuamuru agaregare chini kwenye matope ili kutumikia adhabu
na hatuku elewa kosa nini”Alisema Katarina.
Mkuu huyo wa
Wialaya amewataka wananchi wa Kijiji hicho kutokuwa na mashaka na maisha yao
mara baada ya kuondoka kijijini hapo kwa kutoa taadhari kwa watakao bainika
kuleta vurugu kuchukuliwa hatua mara moja ikiwa ni pamoja na wananchi kuripoti
matendo walio fanyiwa na kiongozi huyo kituo cha Polisi.
|