WAFUGAJI WILAYANI HAI WAJITOKEZA KUPIGA CHAPA MIFUGO YAO.

Katibu Tawala Wilaya ya Hai Upendo Wella akizindua zoezi la upigaji wa chapa kwa Mifugo,zoezi lililo fanyika katika kata ya Kia.

ZAIDI ya Ng’ombe elfu 68 zinatarajiwa kupigwa chapa katika zoezi lililoanza kwenye Halmashauri ya wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro  ili kutekeleza Agizo la wizara ya Mifugo na Uvuvi ambapo linatarajiwa kukamilika Desemba 30 mwaka huu.

Hayo yamebaishwa na Katibu Tawala Wilaya ya Hai Upendo Wella wakati  akizungumza na wafugaji wa kijiji cha Sanya Station Kata ya Kia alipotembelea zoezi hilo pamoja na kufanya uzinduzi huo.

Alisema kuwa kuna kila sababu kwa wakazi wa wilaya ya Hai haswa wafugaji kujitokeza kwa wingi kushiriki zoezi hilo ili kuwezesha wanyama wao kupigwa chapa kutokana na umuhimu wa zoezi hilo

“kukamilika kwa zoezi hili itasaidia kutambua mifugo iliyopo kwani wilaya imekuwa na migogoro ya mara kwa mara kati ya wakulima na wafugaji kutokana na wimbi kubwa la mifugo kutoka wilaya za jirani na hata wafugaji kutoka  nje kuvamia mashamba ya wakulima kwa ajili ya malisho.”Alisema Wella.

Hata hivyo aliwataka wafugaji wote kutoa mifugo yao na kupigwa kwa muda huu na mara baada ya kukamilika kwa zoezi hilo wataanza kuwachukulia hatua wale ambao watashindwa kutekeleza agizo hilo

Kupande wake afisa mifugo wa wilaya ya Hai, Elia Machange amesema kuwa tangu kuanza kwa zoezi hilo wamekutana na muitikio mkubwa kutoka kwa wafugaji ambao wamepeleka mifugo yao kupigwa chapa.

Aidhani amesema kutokana na matumizi makubwa ya kuni wamejipanga kuhakikisha kuwa zoezi hilo halikwami kwa kushirikiana na viongozi wa vijiji kutoa ushirikiano wao wa ili kukabiliana  tatizo hilo na huduma iendeele kutolewa kwa muda wote

Kwa upande wake Mfugaji Yohana Laizer alisema zoezi hilo litasaidia kuwatambua  ngombe watakaovamia maeneo yao kwani mifugo yao itakuwa na chapa ya wilaya ya Hai,huku wizi wa mifugo ukidhibitiwa kwa kiasi kikubwa wakati wa mifugo yao ikihama kutafuta malisho.

Ameongeza kuwa  kupigwa chapa kwa Ng’ombe hao itasaidia kuondoa mwingiliano wa mifugo kwa wilaya nyingine jambo ambalo litawasaidia katika kuhifadhi sehemu za malisho.