APEWA ADHABU YA KIBOKO KIMOJA KWA KUMPA UJAUZITO MWANAFUNZI MWENZAKE.




Hai-Kilimanjaro.

Mahakama ya Wilaya ya Hai Mkoa wa Kilimanjaro imemuhukumu mwanafunzi mmoja wa kidato cha tatu wa Shule ya Sekondari, mwenye umri wa miaka 16 mkazi wa Kikavu chini adhabu ya kuchapwa kiboko kimoja kwa kosa la kumbaka mwanafunzi mwenzake na kumpa ujauzito.


Adhabu hiyo ilitolewa juzi na Hakimu mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo Agness Mhina baada ya kuridhishwa na ushahidi ulio tolewa mahakamani hapo  na mashahidi sita wa upande wa mashtaka.

Akisoma hati ya mashtaka Mahakamani hapo mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo Valeria Banda, alisema kuwa mshitakiwa alifanya kosa hilo siku isiyojulikana mwezi wa oktoba mwaka 2015 maeneo ya Mkalama Wilaya ya Hai ambapo alimbaka mwanafunzi mwenzake wakidato cha tatu na kumpa ujauzito.

Kabla ya hukumu hiyo kutolewa Mwendesha mashitaka Valeria Banda, alidai kuwa vitendo na matukio ya ubakaji yamekuwa yaki tendeka katika jamii,huku jamii ikiwa na uelewa wa kufanya matukio na vitendo hivyo ni kinyume na sheria.

Walio toa ushahidi katika kesi hiyo ni pamoja na Daktari wa hosipitali ya Wilaya ya HAI,Ofisa wa jeshi la Polisi kutoka dawati la jinsi,wanawake na watoto,Mama mzazi wa Mwanafunzi huyo,Mwalimu wa shule anayosoma  pamoja na aliye pata ujauzito.


Aidha Mahakama imetumia  sheria ya alama ya adhabu kutoa hukumu hiyo huku kesi hiyo ikisimamiwa kupitia kifungu cha elimu namba 5 cha sheria ya elimu namba 25 ya mwaka 1978 iliyosomwa, pamoja na gazeti la serikali namba 265 ya tarehe 5 ya mwezi 9 mwaka 2003.