DC HAI:ATOA MUDA WA WIKI MBILI KWA MKANDARASI WA KAMPUNI YA MUGENZO KUKABIDHI KAZI.

Mkuu wa Wilaya ya Hai Gelasius Gasper Byakanwa wa kwanza (Kulia) akimsikiliza Injinia wa Wilaya  Cosmas Peace,aliye vaa kitambulisho,akiongea kwa vitendo,namna ujenzi wa barabara hiyo ulivyo kubalika kufanyika.
Barabara ya Masama Mbweera ikionekana kuchimbwa asubuhi, mara baada ya Mkandarasi wa kampuni ya Mugenzo Company Ltd,kusikia Mkuu wa Wilaya hiyo anaitembelea.

Hai-Kilimanjaro.

Mkuu wa Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro,ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama Gelasius Byakanwa ametoa muda wa wiki mbili kwa  kampuni ya ukandarasi ya MUGENZO COMPANY LTD,          kumaliza kazi alilyo pewa ya ujenzi wa barabara ya Masama mbweera na barabara ya Kyeri machame Magharibi.

Ametoa agizo hilo juzi wakati alipo tembelea barabara hizo mara baada ya kupokea taarifa toka kwa wananchi kuwa ujenzi unao fanywa na Mkandarasi huyo upo chini ya kiwango, mbali na muda alio pewa wa miezi mitatu toka mwaka jana 2016 kuto kukamilika.

“Hatuwezi kuona pesa za serikali zinatumika kumbe zina tumika chini ya kiwango,ni agize ya kuwa Mkandarasi huyu akishindwa kukamilisha barabara hizi asilipwe kiasi chochote ili iwe fundisho kwa Wakandarasi wengine wanao tumia pesa vibaya na kuchelewesha shughuli za kuhudumia wananchi”alisema Byakanwa.

Akitoa ufafanuzi wa ujenzi wa barabara hizo Mhandisi wa barabara Wilaya ya Hai Injinia Cosmas Peace amesema kuwa mkandarasi alipewa tenda hiyo toka mwaka jana akitegemewa kuikamilisha mwezi wa kumi na moja mwaka jana,badala yake alishindwa kufanya hivyo kwasababu zisizo weza kujulikana.

Amesema kuwa ujenzi wa barabara ya Masama Mbweera ulikuwa ni wa kilomita tatu,kwa kiwango cha kushindilia changarawe na barabara ya kyeri kilomita mbili kwa kiwango hicho hicho zote zikiwa na jumla ya shilingi milioni sitini na tano,fedha zilizo toka katika mfuko wa barabara,ambapo mpaka sasa Mkandarasi huyo amesha lipwa shilingi milioni ishirini na mbili laki moja na elfu thelathini.

Katika hatua hiyo Byakanwa amewataka viongozi wa serikali za mtaa kusimamia na kutoa taarifa za kila aina ya ujenzi unaofanyika katika maeneo yao ili kuweza kuwa na miundombinu iliyo kidhi vigezo vinavyo hitajika na Serikali.


“Nasikitika kusikia kuwa Mkandarasi huyu alikuwa kimya pasipo kuendeleza ujenzi huu mpaka pale alipo sikia kuwa nakuja kutembelea barabara hizi ndipo alipo anza kuchimba barabara”Alisema Byakanwa.