DC HAI:ATEMBELEA KAYA MASIKINI KUJIONEA WANACHOKIPATA KUTOKA TASAF.



Mkuu wa Wilaya ya Hai Gelasius Gasper Byakanwa akisalimiana na mtoto kutoka kaya inayo nufaika na ruzuku toka TASAF,Kijiji cha Rundugai alipo watembelea.

Mkuu wa Wilaya ya Hai Gelasius Gasper Byakanwa akioneshwa sehemu ambayo mnufaikaji wa ruzuku toka TASAF,hulala pamoja na familia yake.


Mkuu wa Wilaya ya Hai akizungumza na kaya 91 za watu wanao nufaika na ruzuku toka TASAF,akiwahimiza kukata bima ya afya ili kumudu gharama za matibabu.



Walengwa wa ruzuku toka TASAF wakimsikiliza Mkuu wa wilaya.




Hai-Kilimanjaro.

WANANCHI  wanao nufaika na mpango wa kunusuru kaya masikini Wilayani Hai Mkoani 
Kilimanjaro,wametakiwa kuhakikisha wanatumia fedha wanazopata kukata bima ya afya pamoja na kugawa katika matumizi mengine muhimua na msingi ili kuweza kujikwamua kiuchumi.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Hai Gelasius Gasper Byakanwa wakati alipokuwa akitembelea kaya hizo ili kuhakikisha ikiwa fedha zinazo tolewa na TASAF zinawafikia walengwa kwa wakati na kutumika katika matumizi sahihi.

Amesema kuwa  Mratibu wa TASAF wilaya anapaswa kuhamasisha zoezi la kila kaya kukata bima ya afya ili kuweza kusaidia gharama za matibabu kwa kaya hizo,kwani suala la matibabu limekuwa changamoto kwa walio wengi kushindwa kumudu fedha za matibabu kutokana na kukosa bima ya afya.

Byakanwa ameongeza kuwa kila kaya inayo nufaika na ruzuku hiyo kutoka TASAF zinapaswa kubuni miradi midogomidogo kama vile ufugaji wa kuku,mbuzi, kondoo na bustani za mbogamboga ili kuweza kuzalisha mali itakayo wasaidia kutatua matatizo yao ikiwa mpango huo utafikia tamati,jambo litakalo kuwa lime wajengea uwezo wa kujitegemea.

"Mpaka mwezi wa saba nitakapo kuja tena kuwatembelea nitafurahi kuona kila kaya ina bima ya afya,itakayo wasaidia kupata huduma za matibabu"alisema Byakanwa.


Kwa upande wake Mratibu wa TASAF Wilaya ya Hai Eric Marichamu amesema kuwa, wamepokea fedha za kaya masikini sh 126.4 milioni zitakazo nufaisha vijiji 43 vyenye kaya 3,778 zilizo dhibitishwa kuingia katika mpango huo.