SABABU ZILIZO PELEKEA SHAMBA LA MBOWE KUHARIBIWA MIUNDOMBINU YAKE




picha ikionesha uondoaji wa miundombinu hiyo,kazi iliyo fanywa na Mkuu wa Wilaya hiyo na wakaguzi wa mazingira toka NEMC.




Uwekezaji katika shamba la Kilimanjaro Veggies ulio fanyika ndani ya chanzo cha mto.


HAI-KILIMANJARO

SERIKALI wilayani Hai mkoani Kilimanjaro, imeondoa miundombinu ya
uzalishaji katika shamba la  Kilimanjaro Veggies linalomikiwa na
Mbunge wa jimbo la Hai Freeman Mbowe kutokana na shamba hilo kuwa
ndani ya chanzo cha maji ya mto Weruweru.

Pamoja na kuondoa miundombinu hiyo serikali imemtaka  kulipa kiasi cha
shilingi milioni 18 kutokana na uharibifu wa mazingira aliyofanya
kwenye chanzo hizo pia ametakiwa kulipa gharama zote zilizotumikia
kuondoa miundombinu kwenye shamba hilo.

  Hatua hiyo inakuja baada ya mmiliki wa shamba hilo Freeman Mbowe
kukaidi amri aliyopewa  na serikali ya kusitisha kilimo cha mboga
mboga  katika eneo hilo lenye ukubwa wa hekari mbili lililoko kijiji
cha Nshara ambapo alianzisha shamba hilo kinyume na sheria ya
mazingira.

Mkuu wa wilaya hiyo, Gellasius Byakanwa alisema kuwa wameamua kuondoa
miundombinu yote iliyokuwa ikitumika kwenye shamba hilo baada ya
mmiliki shamba hilo kupewa miezi minne kuondoa kwa hiari yake lakini
alishindwa na kuendelea  kufanya shughuli za kilimo bila kujali amri
ya serikali.

Byakanwa alisema kuwa mnamo Janury 23 mwaka huu Freemani Mbowe alifika
ofisini kwake akiwa na wanasheria wake kutokana  agizo alilotoa kwa
ajili ya kusitisha shughuli za kibinadamu katika shamba ambalo
anamiliki na kukubaliana kuwa atatumia mda wa miezi nne kuondo mazao
yaliyokuwemo kwenye shamba hilo  ambapo miezi minne imeishia Mei 23
mwaka huu.

“Mmiliki shamba hili tulimpa miezi  minne kuondoa mazao yaliyopo
shambani kwake lakini amekaidi amri hiyo pamoja na kwamba anatambua
sheria za mazingira lakini bado aliendelea kufanya shughuli za kilimo
”.

“Huyo ni  kiongozi na ni kiyoo cha jamii haipendezi kufanya vitu kama
hivi,wajibu wa Wananchi kuvitunza vyanzo kwani hakuna mradi utakao
ruhusiwa ndani ya mita 60 kutoka chanzo cha maji,haipendezi hata
kidogo kilimo au kukata miti kwenye vyanzo vya maji”
.
''Sitokubali kuona mazingira yanaharibiwa  katika Wilaya ya hii na
kubaki kuwa jangawa,wakati ndiko kwenye misitu mingi na misitu ndiyo
chanzo kikuu cha kupata mvua ”alisema mkuu huyo wa Wilaya

Nae mkaguzi wa mazingira wa baraza la hifadhi na  mazingira Taifa
kutoka NEMC,kanda ya kaskazini  Novatus Mushi alisema uamuzi huo
unatokana na mmiliki shamba hilo kushindwa kufuata sheria ya mazingira
ya mwaka 2004 kifungu 81 kinamtaka kila mtu anayeanza mradi wa kilimo
kufanya tathinimi ya uharibifu wa mazingira lakini mmiliki huyo
hakufanya na wala hakushirikisha mamlaka husika.

“Mmiliki huyo alikiuka sheria ya mazingira kifungu cha 51 kinachokata
mtu yeyote yule kutokufanya shughuli za mazingira ndani ya eneo  la
mita sitini kando ya chanzo cha maji lakini mtu huyo amefanya hivyo
alivyotakiwa kuondoa amekaidi”alisema.

“Piakifungu namba 200 b cha sheria ya mazingira kinataka mtu yeyote
yule anayepewa mazingizo na mamlaka  za nchi ikiwemo kukataza shughuli
za kibinadamu ndani ya maeneo yanayolindwa kisheria afabye hivyo kwa
kujibu wa muda aliyopewa na mamlaka husika ”alisema.

“Huyo bwana alipewa miezi minne aondoke kwa hiari yake na ofisini ya
mkuu wa wilaya hakufanya hivyo npaka leo hii tunapofanya zoezi bado
shughuli za uzalishaji zilikuwa zikiendelea katika shamba hili kwa
kifupi ni kudharau mamlaka sababu ni mamlaka iliyopo kisheria na
imempa agizo lilipo kisheria.

Pia sisi tulimwandikia barua June 6 mwaka huu ikimkumbusha kuwa
asitishe shughuli za kibinadamu katika eneo hilo ambayo iliambatana na
adhabu ya kumtaka kulipa kiasi cha shilingi milioni 18 kutokana
uharibifu wa mazingira katika chanzo hicho maji cha mto Weruweru
”alisema.