SOMENI MKIMUOMBA MUNGU AWAFANYIE WEPESI


Image result for wanafunzi wakisoma


Hai-Kilimanjaro.
 Wanafunzi wa shule za sekondari  nchini wametakiwa kusoma kwa bidii pamoja na kumcha Mungu ili waweze kufanikiwa katika masomo yao na kufanikisha ndoto zao za kielimu kama vile vitabu vya dini vinavyo wataka kushika elimu.

Wito huo ulitolewa  na Diwani wa Kata ya Masama Mashariki mheshimiwa John Munis wakati alipotembembelea shule mbili za sekondari  zilizopo katika kata yake ambazo ni Marire  na Sawe na kuwapongeza waalimu kwa kufundisha kwa bidii pamoja na wanafunzi waliofaulu vizuri katika masoma mbalimbali.

Akikabidhi zawadi kwa wanafunzi hao mh Munisi alisema kuwa anatambua jitihada zinazofanywa na waalimu hao katika kufanikisha ufaulu,na kuwataka wanafunzi wote kuongeza bidii katika masomo na kuwaahidi kuwa wanafunzi wote watakaofaulu kwa daraja la kwanza watapata zawadi bila kujali wingi wao.

Alisema kuwa kila mmoja akitambua wajibu wake akiwemo mzazi, mwalimu na mwanafunzi  ufaulu utaongezeka kwa asilimia kubwa na kusisitiza kila mmoja kutenda kwa haki .
Kwa upande wake diwani wa kata ya Machame Uroki Robsoni Kimaro  aliwapongeza waalimu wa shule hizo kwa kufundisha kwa bidii bila kujali changamoto wanazokutana nazo  huku akiwataka wanafuzi  kuongeza bidii ya kusoma pamoja na kuepuka  matendo maovu ikiwepo ngono na unywaji wa pombe.


Nae mwenyekiti wa bodi ya shule ya marire Dkt Abisai Masawe  na Mkuu wa shule hiyo mwalimu Namkanda Kagonji amewashukuru madiwani hao kufika katika shule zao huku wakihaidi kutekeleza mikakati yote waliyoipanga.