Taarifa ya msiba mkubwa kwa wanatasnia ya habari Mkoani Kilimanjaro na Taifa Kwa Ujumla.

Picha ya Gari walilokuwa wakisafiria Kutoka Rombo kurudi makwao mara baada ya kupata ajali eneo la Mwika Mawanjeni.

From Media Club Of Kilimanjaro.


Taarifa ya msiba mkubwa kwa wanatasnia ya habari Mkoani Kilimanjaro na Taifa Kwa Ujumla.

Watu saba wamekufa papo hapo katika ajali iliyo tokea eneo la Mwika Mawanjeni maarufu kama “Baa mpya” akiwemo wanahabari wa magazeti ya serikali na Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Hai,Arnold Swai.

Swai na wenzake walikuwa wakitokea katika sherehe ya miaka 40 ya CCM ambayo kwa Mkoa wa Kilimanjaro ilifanyikia Wilayani Rombo.

Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama na Mkuu wa wWlaya ya Rombo,Agnes Hokororo alisema ajali hiyo ilitokea katika eneo hilo na kuhusisha magari mawili pamoja na pikipiki moja.

Wengine waliyo fariki katika ajali hiyo ni pamoja na Anastazia Malaysia ambaye ni Mwenyekiti wa UWT Tawi la Chuo kikuu Cha Ushirika Moshi(MOCU) Na mkazi wa Shimbi,Rombo na Edwin Msele Katibu wa hamasa shirikisho la Vyuo vikuu Moshi Mjini.

Wengine ni Ally Mbaga(Mjumbe wa NEC) Wilaya ya Same na mkazi wa Mwanga,mwanamke ambaye alikuwa katika bodaboda ambapo Fuso liligonga pikipiki hiyo na mtu mwingine ambaye hajafahamika mara moja.

Hokororo amesema kuwa majeruhi ni Mwnahabari Jackson Kimambo aliye kuwa anaendesha gari aina ya Toyota Surf,ambapo hali yake inaendelea vizuri akipatiwa matibabu hosipitali ya rufaa ya KCMC ambapo Miili ya marehemu wote imehifadhiwa chumba cha kuhifadhia maiti katika hosipitali hiyo.

Taarifa za awali kutoka eneo la tukio zinaeleza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni kuwa gari aina ya fuso lilifeli breki na kugonga gari hilo kwa nyuma kabla ya kuiparamia na kuigonga pikipiki na kusababisha vifo hivyo.


Kamanda wa Polisi Mkoani Kilimanjaro anatarajia kukutana na waandishi wa  habari leo kuzungumzia tukio hilo.