UHARIBIFU WA MAZINGIRA CHANZO CHA UKOSEFU WA MAJI WILAYANI HAI.


Picha ikionesha uharibifu wa mazingira unaofanywa na wakazi wa Wilaya ya Hai Kata ya masama kati na Masama Mashariki katika mto Namwi ulio tegemezi kwa wakazi waishio tambarare
Wananchi waliojitokeza kupanda miti katika mto Namwi wakimsikiliza Diwani wa Kata ya Masama Kati,wakati akiwapongeza kwa zoezi hilo muhimu la kunusuru mazingira.

Picha ikionesha bonde la mto Namwi na miti iliyo pandwa na wananchi.


Hai-Kilimanjaro

CHANZO cha uharibifu wa mazingira katika mto Nawi uliopo katika kijiji
cha Nguni Wilayani Hai mkoani Kilimanjaro imeelezwa kuchangia
kukosekana  kwa maji katika maeneo ya ukanda wa tambarare katika
wilaya hiyo.

Uharibifu huo ambao umefanywa na baadhi ya wananchi kwa kufanya
shughuli za kinadamu bila kujali  madhara ya shughuli  wanazozifanya
kumepelekea wananchi kukosa maji kwa ajili ya matumizi ya nyumbani
pamoja na kukwamisha kilimo cha  umwagiliaji .

Akizungumza katika zoezi la upandaji miti katika mto huo , diwani wa
kata ya Masama kati Deogratius Kimaro  alisema shughuli za  kibidamu
zinazofanywa katika mto huo unaotegemewa kupelekea maji kwa wananchi
wanaoishi ukanda wa tambarare na  kukosa maji hali ambayo imepelekea
kupungua kwa maji  na kushindwa kufanya shughuli nyingine za
uzalishaji.

“Ndugu wananchi shughuli mnazofanya katika mto huo zimesabisha madhara
makubwa kwa wakazi wa ukanda wa tambarare na hata sisi wa ukanda huu
kwani maji ni machache kwenye  mto huu kutokana na sisi mwenyewe
kulima kwenye vyanzo pamoja na kukata miti ambayo ilisaidia kuboresha
uoto wa asili” alisema Kimaro.

Alisema , jukumu la utunzaji wa mazingira ni la kila mmoja na kuondoa
dhana iliyojengeka miongoni mwa baadhi ya jamii kuona kuwa zoezi la
utunzaji  wa mazingira ni la serikali kitu ambacho si sahihi na
kuwataka kuondokana na dhana hiyo.

Nae mkazi wa kijiji hicho Onesmo  Kileo alisema kuwa shughuli za
kibinadamu zinaendelea katika vyanzo vya maji kutokana na dhana
iliyojengeka kwenye jamii kuwa maeneo hayo ni ya urithi na
wanayamiliki kihali na kuamua kufanya shughuli hizo.

Kwa upande wake ofisa misitu wa kata, Masama Mashariki John  Katikirwa
, alisema wanakabiliana changamoto kubwa katika zoezi la kudhibiti
hali ya uharibifu wa mazingira kutokana na baadhi ya viongozi
kushirikiana na watu wanaohusika na uharibifu  mazingira.

Hata hivyo Katikirwa alisema zoezi la upandaji wa miti litakuwa
endelevu kwa lengo la kurudisha hali ya uoto wa asili uliopotea
kutokana na baadhi ya watu kukata , kulima  na kuchoma miti katika

maeneo yalitengwa kwa ajili ya utunzaji wa mazingira