Wilaya ya Hai


Mahali pa Hai (kijani) katika mkoa wa Kilimanjaro.
Wilaya ya Hai ni wilaya moja ya Mkoa wa Kilimanjaro. Katika sensa ya mwaka 2002, idadi ya wakazi wa Wilaya ya Hai ilihesabiwa kuwa 210,533.[1]
Katika wilaya hiyo wakazi wengi ni Wachaga ambao huzungumza lahaja tofauti, kama Wamachame na Wamasama.

WIlaya hii ilitengwa mwaka 1975 kutoka Wilaya ya Moshi ya awali. Imepakana na Wilaya za Moshi Vijijini (mashariki), Arusha Vijiini na Siha (magharibi). Simanjiro (kusini), Rombo na Mbuga wa Kilimanjaro upande wa kaskazini.
Eneo lake ni kilomita za mraba 1,011. Kiutawala imegawiwa kwa tarafa 3 (Lyamungo, Machame na Masama), kata 14 na vijiji 60. Idadi ya vitongoji ni 248.
Kuna kanda 4 zenye tabianchi tofauti maana wilaya iko kenye mtelemko wa Mlima Kilimanjaro[2]
  • Kanda ya Kilele cha Mlima iko juu ya kimo cha mita 1,800 UB pamoja na kilele cha Kibo. Ni hasa maeneo ya mbuga na hifadhi ya taifa hivyo hakuna wakazi wa kudumu. Ni asilimia 27 za eneo la wilaya.
  • Kanda ya Juu: iko kwenye kimo kati ya mita 1,666 na 1,800 juu ya UB. Inafaa kwa kilimo cha kahawa na ndizi. Walio wengi ni wakulima wadogo wanaofuga pia ng'ombe wa maziwa na kuuza maziwa.
  • Kanda ya Kati: iko kwenye kimo kati ya mita 900 hadi 1,666 juu ya UB. Inapokea mvua kati ya milimita 700 hadi 1250 kwa mwaka; kilimo inafanana na kanda ya juu.
  • Kanda ya Chini iko kwenye kimo chini ya mita 900 juu ya UB. Hapa mvua inapungua hadi milimita 500-700 kwa mwaka. Mazao yanayostawi ni pamoja na maharagwemahindializeti na mpungaUfugaji hapo chini si hasa ya maziwa ni zaidi ng'ombe wa kienyeji.