DC HAI: TUMIENI KOMPYUTA KWA MALENGO MAHUSUSI,ZITA WASAIDIA.

Mkuu wa Wilaya ya Hai Gelasius Byakanwa (kushoto) akipoke kompyuta toka kwa Mkurugenzi wa NMB Tanzania Bi.Ineke Bussemaker (kulia) katika tukio la Benki hiyo kutoa Kompyuta saba kwa shule ya sekondari maili Sita,anaye fuata ni Katibu Tawala Wilaya Upendo Wella  akifurahia.
HAI-KILIMANJARO.

Serikali Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro imepongeza Benki ya NMB Tanzania kwa kuamua kuisaidia shule ya sekondari maili Sita kuwa sehemu ya shule iliyo pokea kompyuta saba kwaajili ya kukuza teknolojia ya mawasiliano shuleni.

Pongezi hizo zimetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Hai Gelasius Byakanwa wakati akipokea kopyuta saba toka kwa Mkurugenzi wa Benki ya NMB Tanzania Bi.Ineke Bussemaker.

Amesema kuwa ulimwengu wa sasa pasipo kuwepo na vifaa bora vya mawasiliano dunia haito weza kuwa ya kisasa kama inavyo hitajika hivyo kuwataka wanafunzi wa Shule hiyo pamoja na Waalimu kuweza kutumia vifaa hivyo kwa makini ikiwa ni pamoja na kutumika katika malengo mahususi.

“Niombe sana vifaa hivi vitumike kwa malengo maalumu yatakayo weza kujenga kizazi kizuri chenye faida kwa Taifa,sitegemei kusikia kuwa vifaa hivi vitatumika kufanya mambo yatakayo bomoa maadili na malengo mahususi”.Alisema Byakanwa.
Byakanwa ametaka uongozi wa shule hiyo kuanza kutumia kompyuta hizo kwa kutumia waalimu waliopo shuleni hapo wenye uelewa wa kutumia vifaa hivyo,wakati wakisubiri waalimu wa masomo hayo kupangwa kuja shuleni hapo.

Ameongeza kuwa ofisi yake kwa kushirikiana na Afisa elimu watashughulikia upatikanaji wa waalimu walio fuzu kufundisha mambo ya mawasiliano watakao tumika katika shule hiyo kutoa elimu kwa wanafunzi na zoezi la kuwapata waaalimu hao halita zidi miezi mitatu.

Aidha ametoa agizo kwa shule zote za sekondari pamoja na bodi za shule  kuhakikisha kuwa wanaandika majina ya watoto walio fanya vizuri  kwenye kuta na vibao katika shule zao ili kuweza kuongeza chachu ya ufaulu kwa wanafunzi kushindania kwa majina yao kubaki kumbukumbu.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa NMB Tanzania Bi.Ineke Bussemaker    amesema kuwa Benki ya NMB inatambua umuhimu wa elimu katika kumfanya Kijana wa sasa kuwa kijana  mzuri kwa manufaa ya kesho kwa kumjengea uwezo katika teknolojia ya mawasiliano.


Ameongeza kuwa elimu inasaidia kuhakikisha kuwa taifa linaendelea kwa kupitia mchango wa elimu hivyo kuwataka wanafunzi hao kuhakikisha kuwa wanatumia muda wao vizuri ili kuweza kufikia malengo ya mmoja moja  na Taifa.