DED HAI:AFURAHIA NJIA MPYA YA KUSIKILIZA NA KUTATUA KERO ZA WANANCHI WA HAI.ASEMA NJIA HIYO ITASAIDIA KULETA MAREKEBISHO NA MAENDELEO


Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Hai Yohana Sintoo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai anawatangazia Wananchi na Watumishi wote kuwa dawati la malalamiko alilo anzisha litafanya kazi ya kupokea na kutatua kero mbalimbali.

Ofisi ipo wazi siku ya Jumanne na Alhamisi saa tatu akamili asubuhi hadi saa tisa na nusu alasiri kweye ofisi ya kero iliyopo katika Ukumbi wa Maktaba ya Hai.

Vile vile Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai atakuwa akipokea kero na kutoa majibu yake kupitia Redio Boma Hai Fm siku ya Ijumaa saa kumi na moja jioni kupitia kipindi cha Drive Home.

Aidha,mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai anapenda kuwahakiiishia kuwa uwepo wa usiri wa kero na taarifa zitakazo pokelewa.

Pia mlalamikaji anaweza kuwasilisha malalamiko yake kwa njia ya barua na atume kwa Mkurugenzi Mtendaji.
S.L.P 27,Hai
Fax:+255-272758441
Email:Mkurugenzihai@yahoo.com
Imetolea na:
Ofisi ya Mkurugenzi MTENDAJI (W)

Hai.