Mkuu wa Wilaya ya Hai Gelasius Byakanwa akitoa maagizo kwa bodi ya vyama vya ushirika vilivyo shindwa kujiendesha na kuwa na wawekezaji. |
SERIKALI
Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro imetoa miezi mitatu kwa bodi za vyama vya ushirika
vilivyo shindwa kulipa kodi,kutafuta wawekezaji katika mashamba yaliyo wazi na
mashamba yenye migogoro kutatua changamoto hizo kabla serikali haija futa
kibali cha mashamba hayo.
Akizungumza
wakati wa kikao na viogozi wa bodi wa vyama vya ushirika wilayani Hai,Mkuu wa
Wilaya ya Hai Gelasius Byakanwa amesema kuwa serikali inataka kuona mashamba
hayo yakifanya kazi huku yakitoa ajira kwa wananchi pamoja na serikali
kunufaika na kodi ili kuongeza patoa la Nchi.
Amesema kuwa
yapo baadhi ya mashamba mengine ambayo yana migogoro na wawekezaji hivyo kuleta
hali ya kusuasua kwa wawekezaji hao kuanza kufanya kazi huku muda wa mkataba wa
makubaliano ukimalizika hivyo kuwataka kumaliza migogoro hiyo na mashamba hayo
kuanza kufanya kazi mara moja.
Byakanwa
amesemea kuwa kwa bodi ambazo wawekezaji wake wamefanya mabadiliko ya kugawa
shamba kwa mwekezaji mwingine bila kufuata taratibu,bodi hizo kujisalimisha
zenyewe kwa kamishina wa ardhi ambayo ni mahakama ili taratibu za kisheria
ziweza kufuatwa.
Aidha
amesikitishwa na baadhi ya bodi za vyama vya ushirika kutelekeza mashamba yao
pamoja na miundombinu kuharibiwa ikiwemo shamba la Silver day na mbono na kuta
kila bodi kuweza kushughulikia tatizo hilo ndani ya miezi mitatu aliyotoa.
Kwa upande
wake Diwani wa kata ya Masama Magharibi Harison Masakia amemtaka mkuu wa wilaya
hiyo kutazama suala la wawekezaji akiwemo mwekezaji wa Bondeni estate na
Nkwansra estate ambao wamebadilisha matumizi na sheria ya uwekezaji kwa kufuga
mifugo badala ya kilimo huku wengine wakikodisha mashamba hayo kwa wananchi
jambao ambalo ni kinyume.
Naye Shila
Steven uronu Makamu mwenyekiti wa shamba la Nshara Amkosi Makuru amekiri kuwa
wakati wa kukabidhiwa mashamba hayo hawakupata miongozo huku wengine wakivunja sheria zilizo kuwa
katika makabidhiano ya mashamba hayo,hivyo kumuomba Mkuu huyo wa Wilaya kutoa
muda ili vyama hivyo viweze kujirekebisha kutokana na mapungufu makukbwa kuwepo
katika vyama hivyo.