PICHA ya maktaba ikiwa onesha Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Kilimanjaro wakiwa katika ziara ya Kupanda mlima Kilimanjaro. |
MOSHI
CHAMA cha
Waandishi wa habari Mkoani Kilimanjaro MECKI
kinatarajia kuzindua kampeni maalumu ya kimkoa ya kukabiliana na matukio
ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kukatishwa masomo kwa kupewa
ujauzito.
Kampeni hiyo
inatarajiwa kuanza septemba mosi hadi 31 mwaka huu kwa kuwashirikisha waandishi
wote wa mkoa bila kujali wanachama na wasiyo wanachama wa klabu hiyo na
kuzinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira.
Mwenyekiti
wa Kampeni hiyo yenye ujumbe ELIMU YAKE KWANZA UZAZI BAADAE,NakaJumo James
amesema kuwa malengo makuu ni kuokoa
kundi kubwa la wasichana wanao katishwa masomo kwa kupewa ujauzito huku
watuhumiwa wakitumia mbinu kukwepa mkono wa sheria.
James ameema
kuwa tatizo hilo linaonekana kuzidi kuwa kubwa hivyo kutakiwa kuchukuliwa uzito
wa kutosha katika kutatua tatizo hilo ambapo elimu ya mtoto wa kike ipo
mashakani na kutolea mfano wa wilaya za Rombo na Same pekee,zaidi ya wananfunzi
144 wamepata ujauzito kuanzia januari hadi Agost mwaka huu.
Ameongeza
kuwa kwa mujibu wa Afisa Elimu sekondari wilaya ya Same Happines Laizer na
washule za Msingi wilayani humo Amri Msemo amesema kuwa wilaya hiyo ina wanafunzi
54 waliyopea ujauzito huku 52 wakiwa ni
sekondari na 2 shule ya msingi.
Kwa upande
wa Wilaya ya Rombo,kwa mujibu wa Katibu Tawala wake Abubakari Asenga ameema
kuwa hadi kufikia Julai tayari kuna
wanafunzi 90 ambao wamepewa ujauzito.
Mapema
Katibu wa kampeni hiyo,Abdalah Husein
amesema kuwa Kmapeni itafungwa na kiongozi wa Kitaifa ambaye atatangazwa
baadae huku wakuu wote wa Wilaya wakiombwa kutoa elimu kwa jamii hususani
Wanafunzi,wazazi,walezi na wadau wengine muhimu.