Mkurugenzi wa Halimashauri ya Wilaya ya Hai Yohana Sintoo,akisifu ubora wa mazingira katika bodi ya maji Losaa Kia katika chanzo cha maji Ulengu kilichopo Kata ya Masama Mashariki. |
Mkurugenzi wa Halimashauri ya Wilaya ya Hai Yohana Sintoo,akipanda mti aina ya Mti karanga katika bodi ya maji Losaa Kia katika chanzo cha maji Ulengu kilichopo Kata ya Masama Mashariki. |
Afisa misitu kata ya Masama Mashariki John Katikiro akipanda mti katika bodi ya maji Losaa Kia katika chanzo cha maji Ulengu kilichopo Kata ya Masama Mashariki. |
Mtambo unao tumika kuweka kiwango cha dawa ya kutibu maji katika bodi ya maji Losaa Kia katika chanzo cha maji Ulengu kilichopo Kata ya Masama Mashariki. |
Mhasibu wa bodi ya maji Losaa Kia Senyaeli Nko akisoma risala katika bodi ya maji Losaa Kia katika chanzo cha maji Ulengu kilichopo Kata ya Masama Mashariki. |
Mkurugenzi
mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Hai ndugu Yohana Sintoo ameipongeza bodi ya maji Losaa Kia kwa utunzaji bora wa
mazingira huku pia akiahidi kutumia sheria za maji katika kulinda rasilimali
maji ambayo ni muhimu kwa uhai wa binadamu.
Sintoo
ameyasema hayo hii leo katika chanzo cha maji cha Ulengu ikiwa ni mwendelezo wa
wiki ya maji ambapo amesema kuwa ili kutatua changamoto zilizopo ni vyema
sheria zikafuatwa pasipo kumuogopa mtu yeyote.
Sanjari na
hayo mkurugenzi ameagiza uongozi wa bodi hiyo ya maji kufuatilia madeni kwa
wateja sugu ikiwa ni njia ya kuzikabili changamoto zilizopo ambapo pia kupitia
madeni hayo yatasaidia kupanua miundo mbinu ya maji.
“Niagize
bodi za maji kuhakikisha kuwa wana kusanya madeni yote yalio nje kwa wateja
ambao ni wadaiwa sugu,ambao wamekuwa mapapa,wakidaiwa kila siku pasipo
kulipa,msiwafumbie macho wachukulieni hatua za kisheria maana hao ni wahujumu
maji”alisema Sintoo.
Moja ya
changamoto kubwa inayoikabili bodi hiyo ya Losaa Kia ni pamoja na ongezeko la
watu ambapo awali mradi huo ulitegemewa kuhudumia watu wasiozidi elfu sitini na
sasa mradi huo unahudumia watu zaidi ya elfu sabini.
Kwa upande
wake Mhasibu wa bodi ya maji Losaa Kia Senyaeli Nko kwa niaba ya Mwenyekiti wa
bodi ya maji wilaya Epafra Urassa amesema kuwa bodi hiyo ya maji imekuwa
ikikabiliwa na changamoto lukuki ikiwemo uharibifu wa mazingira unao fanywa na
binadamu ikiwemo kulima katika vyanzo vya mito na chemichemi ,kukata miti
rafiki kwa mazingira pamoja na kuharibu miundombinu ya maji jambo linalo
pelekea maji kupungua.
“Tunasikitika
kuona kuwa uharibifu huu unafanywa na wananchi ambao wanayo elimu ya umuhimu wa
utunzaji wa mazingira,nah ii ni hatari kwa usambazaji wa maji kwani kiwango
kilicho kusudiwa kupelekwa kwa wananchi kinapungua.”Alisema Nko.
Wiki ya maji
inaendela na inatarajika kukamilika wiki hii ambapo maadhimisho yake katika
mkoa wa Kilimanjaro yatafanyika hapa
wilayani Hai huku wiki ya maji ikienziwa kwa upandaji miti katika vyanzo vya
maji na kauli mbiu ikiwa ni “PANDA MITI KUTUNZA VYANZO VYA MAJI”.
Picha na Haikaziblog.