Mkuu wa wilaya ya Hai Gelasius Byakanwa akifurahia kukata keki, katika siku yake ya kuzaliwa leo.
|
DED HAI: Yohana Sintoo Akifurahia keki ya Mkuu wa Wilaya katika kumbukumbu yake ya siku ya kuzaliwa. |
|
Watumishi wa halmashauri ya Hai wakifurahia keki. |
Leo septemba 19 Mkuu wa
Wilaya ya Hai Gelasius Byakanwa amefurahia siku yake ya kuzaliwa na watumishi
wake wa halmashauri.
Katika kusherehekea siku hiyo
ame nukuliwa akisema maneno haya.
“Kwa wale ambao wamebahatika kuwa na mama zao
mpaka hivi sasa wamshukuru Mungu na wawapende sana mama zao.Mimi binafsi
nilimuambia mama yangu kuwa sita weza kumuangusha katika jitihada zangu za
kutafuta maisha na sipo tayari kushindwa na jambo lolote.Nashukuru mama yangu
alinielewa na niliweza kumuhakikishia hilo.
Tenga muda wa kukaa na mama
yako umpe faraja na kumsikiliza pale anapo hitaji msaada wako.Akina mama
wamekuwa wakifanya kazi ngumu na za hatari sana katika kuwakuza watoto
wao,ukipata nafasi jaribu kumkumbuka walau apate faraja na wale wasiyo na mama
wapate nafasi ya kumshukuru Mungu na kumuombea mama alale mahali pema.” Alisema
Byakanwa.
|