Kiwanda cha African Vegetables kilichopo Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro. |
HAI-KILIMANJARO
Mwekezaji wa
kiwanda cha African Vegetables kilichopo Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro Andry
Emmanuel,ametakiwa kutoa uthibitisho wa uwekezaji wake kuwa chini ya
EPZA,kutokana na kuonekana kuwa hauja kidhi vigezo vinavyo takiwa na EPZA.
Agizo hilo
limetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Hai Gelasius Gasper Byakanwa wakati alipo
tembelea bodi ya shamba la Nshara Amcos
saccos katika eneo la Makuru Estate linalo simamiwa na chama hicho.
Amesema kuwa
mwekezaji huyo kulipa kodi isiyo endana na uwekezaji wake huku akiwa amefutiwa
kodi ni jambo lisilo kubalika na
serikali kutokana na mapato ya serikali kupotea bila sababu ya msingi.
“kwa kuonesha
kuwa yupo chini ya EPZA na kulipa kodi ya shilingi laki saba na sitini na tano
jambo hili siyo sawa tena ukizingatia ni kwa ukubwa wa eneo la ekari 471,Kumuita
mwekezaji anafaaa kuitwa hivyo laikini siyo kwa daraja la EPZA,kama analipa
kodi ya kuanzia milioni hamsini na kuendelea,angalau serikali ingekuwa inapata
hizo pesa ange kubaliwa kuwa chini ya EPZA”alisema Byakanwa.
Byakanwa
alitoa ufafanuzi kuwa wawekezaji walio chini ya EPZA wanapaswa kuhakikisha kuwa
wameajiri idadi ya watu wengi ambao wanaweza kupata ujuzi na maarifa kipindi
chote wawapo kazini,kampuni kuwa na uwezo wa kuzalisha kuanzia tani nne na
kuendelea ambapo serikali ndipo huwa futia kodi kwa miaka kumi kutokana na
mchango wao kuonekana na kutambulika.
“Inashangaza
kuona kuwa kampuni hii ipo chini ya EPZA
lakini uzalishaji wake ni mdogo kwani wanauwezo wa kuzalisha tani moja na huku
idadi ya wafanyakazi wakiwa hamsini,pasipo wafanyakazi hao kuto kupata ujuzi
kama EPZA inavyo taka,kwani kazi waliyo nayo ni kuchemsha maharage wanayo
zalisha katika kampuni hiyo tu”.
Katika hatua
hiyo Mkuu huyo wa Wilaya alimtaka mwekezaji huyo kufika ofisini kwake kabla ya
tarehe 2 mei mwaka huu mara baada ya mwekezaji huyo kurudi toka safarini, akiwa
na vigezo na viambatanisho vinavyo muonesha kuwa yupo chini ya EPZA kihalali.
Kwa mujibu
wa maelezo ya Meneja wa Kampuni hiyo Rudy Asukile amesema kuwa uzalishaji wa
kampuni hiyo hauja fikia kiwango cha kuwa chini ya EPZA kama inavyo takiwa
kutokana na uzalishaji kuwa mdogo.
Kwa upande
wake Mwenyekiti wa Nshara Amcos Saccos Abick Uronu amesema kuwa, kwa kipindi
cha mwaka 2016-2017 mwekezaji huyo anadaiwa kiasi cha shilingi milioni 81
ambazo alipaswa kulipa toka Julai 1. 2016,jambo linalo pelekea kukwamisha
shughuli na utekelezaji wa miradi ya jamii na chama kama ilivyo kusudiwa.
Kampuni hiyo
inahusika na usindikaji wa maharage mabichi ambayo husafirishwa nje ya nchi
kipindi chote cha uzalishaji wa nafaka hiyo.