VIONGOZI wa
madhehebu ya dini wametakiwa kufanya kazi kwa bidii ili kujiongezea kipato na
kuacha tabia ya kutegemea sadaka zinazotolewa na waumini
kuendeshea maisha yao
Wito
huo umetolewa na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya Hai mkoani
Kilimanjaro , Yohana Sintoo wakati akizungumza na viongozi wa Bazara la
makanisa ya Kipentekoste mkoani hapa (C.P.C.T) walipokutana katika kanisa na
T.A.G Elishadai Bomang’ombe
Alisema
viongozi wa dini wanatakiwa kuwa mfano mzuri katika kufanya kazi zinazozalisha
na kuacha tabia kutegemea sadaka inayopatikana kwenye makanisa hayo jambo
ambalo limechangia kuwepo kwa migogoro ya kidini pindi hali ya mapato
inapopungua .
“Viongozi
wa dini mnatakiwa kuwa mfano mzuri kwa jamii mnayoiongoza kwa kufanya kazi kwa
bidii na kuepukana na kutegemea sadaka pamoja na misaada kwa kufanya
hivyo mtakuwa mfano mzuri kwenye jamii” alisema Sintoo
''Kuna
baadhi ya viongozi wa dini hawataki kujishughulisha kwa kufanya kazi hata
kidogo kazi yao kubwa ni kusubiri sadaka kutoka kwa waumini wao hauipendezi
tunatakiwa kufanya kazi ili kupeleka watoto wetu shule''alisema
“Pamoja
na kuwatunza watu kiroho ni lazima tujishughulishe kwa shughuli nyingine
za uzalishaji pamoja na kuwaendeleza watoto wetu kielimu haipendezi kuona
mtoto wa mchungaji akiwa anazurura mtaani kwa kukosa ada ya shule ” alisema
“
Tunategemea viongozi wa dini wawe mfano wa kuigwa kwa kufanya matendo mema,
kujishughulisha na kuendeleza watoto wao pamoja na kuwafundisha waumini waumini
wao namna ya kujikwamua kiuchumi ”
“
Rais wetu John Pombe Magufuli ameshatoa maelekezo kuwa watu wote wafanye kazi,
tena wafanye kazi kwa nguvu zao zote ili kujiongezea kipato kwa familia na
Taifa kwa ujumla''alisema Sintoo,
Alifafanua kuwa Serikali inatambua mchango mkubwa wa Viongozi wa dini katika kupunguza Imani potofu, na kutatua migogro ndani ya familia na jamii kwa ujumla, hivyo huchangia kupunguza vitendo viovu katika jamii.
Awali
akisoma risala ya baraza hilo , mchungaji Werande Munis, alisema lengo la
kusanyiko hilo ni kufanya ibada ya pamoja na kufahamiana ili kudumisha
ushirika wa watumishi wa Mungu katika wilaya hiyo
Hata
hivyo baraza hilo linatoa pongezi za dhati kwa Rais Jamhuri wa Muungano wa
Tanzania , John Pombe Magufuli kwa jitihada zake za kufufua uchumi na kutetea
maslahi ya Taifa na watu wake kwa uzalendo na ujasiri.