HAI-KILIMANJARO
SERIKALI mkoani Kilimanjaro imesema kuwa hatua
zilizochukuliwa na mkuu wa wilaya ya Hai Gellasius Byakanwa za kuondoa
miundombinu ya umwagiliaji katika shamba la Kilimanjaro
Veggie si za kisiasa bali ni taratibu za kisheria za kulinda vyanzo vya maji.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghira alitoa kauli hiyo wakati alipotembelea shamba hilo lililopo
kijiji cha Nshara ili kujionea hali halisi ya uharibifu wa mazingira uliofanywa katika eneo hilo linalomikiwa na mbunge wa jimbo la Hai, Freeman Mbowe.
Alisema hatua zilizochukuliwa na mkuu wa wilaya ya Hai
pamoja na mamlaya ya kusimamia mazingira (NEMC)ni hatua sahihi za kulinda
vyanzo vya maji pamoja na uoto wa asili kwa mujibu wa sharia ya mazingira ya
mwaka 2004 .
Alifafanua kuwa endapo mazingira yatatunzwa vizuri kila kitu
kitafanyika kwa ufasaha na kutokutunza mazingira kumechangia kupelekea kuwepo
kwa migogoro ya mara kwa mara kutokana na kutegemea sana utunzaji vyanzo vya
maji katika kutunza mazingira .
Hata hivyo Mghira alisisitiza
kutokuendelea kwa shughuli zozote za kibinadamu katika shamba hilo kwani
mmiliki alikwisha kiri kufanya kosa na kupewa adhabu ya kulipa kiashi cha
shilingi milioni 18.
Nae diwani wa kata hiyo, Clement Kwayu alimwomba mkuu wa
mkoa kuruhusu kuendelea kwa kilimo hicho katika eneo hilo kwa kimesadia kutoa
ajira kwa vijana zaidi ya 50 na pia eneo hilo ni la
asili wameweza kulima zaidi ya miaka 40.
Nae mkaguzi wa mazingira wa baraza la hifadhi na
mazingira Taifa kutoka NEMC,kanda ya kaskazini Novatus Mushi alisema uamuzi wa Mmiliki wa shamba hilo umekiuka sheria ya mazingira kifungu cha 51 kinachokata mtu yeyote
yule kutokufanya shughuli za mazingira ndani ya eneo la
mita sitini kando ya chanzo cha maji.
mita sitini kando ya chanzo cha maji.