Mkuu wa Wilaya ya Hai Gelasius Byakanwa wa kwanza upande wa ( kulia) akipata maelekezo ya njia ya kupandikiza mmea huo(Macadamias) toka kwa mwekezaji wa shamba hilo la Mbosho Coffee,James Paul. |
Mkuu wa Wilaya hiyo Gelasius Byakanwa pamoja na Katibu Tawala Wilaya Upendo Wella,wakisoma maelezo ya nafaka ya Academia mara baada ya kupakiwa katika mifuko tayari kwa matumizi. |
Pichani ni zao la Macadamias (karanga mti) mara baada ya kuvunwa tayari kwa maandalizi ya kuikoboa na kupata kiini cha ndani ambacho ndicho kinacho hitajika. |
Hai-Kilimanjaro.
Wananchi Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro,wameshauriwa kuanza kulima zao la biashara aina ya Macadamias alimaharufu kama karanga mti ili kuweza kuongeza kipato
chao,kutokana na zao hilo kuwa na uhitaji mkubwa katika masoko ya ndani na nje ya
nchi .
Rai hiyo
imetolewa leo na Mkuu wa Wilaya ya Hai Gelasius Gasper Byakanwa wakati
alipotembelea shamba la Mbosho Coffee linalo milikiwa na muekezaji James
paul,kwa lengo la kupata ufafanuzi wa zao hilo la biashara ili kuweka utaratibu
wa wananchi kushauriwa kulima zao hilo.
Amesema kuwa
kutokana na Mwekezaji huyo kuanza kuzalisha zao hilo ambalo linahitajika sana
kwa masoko ya nje,kutokutosheleza lengo la wateja,ni vema wananchi kujipanga
kulima zao hilo pindi taratibu zitakapo kamilika sambamba na ushauri toka kwa
wataalamu wa kilimo wilaya.
“Nimevutiwa
sana na muwekezaji huyu kwa zao lake hili,vilevile nimependezwa na mpango wake
wa kutaka kuwashirikisha wananchi kulima zao hili ili watu weyu wapate faida”alisema Byakanwa.
Byakanwa
ameongeza kuwa,mara baada ya kumalizika ushirikishwaji kwa pande zote zinazo
husika katika masuala ya kilimo,wananchi watapata fursa ya kupewa elimu ili
kuanza zao hilo lenye kipato kikubwa mara moja.
Kwa upande wake
mwekezaji huyo James Paul,amemshukuru Mkuu wa Wilaya kwa kutembelea shamba hilo ikiwa ni pamoja na
kusikiliza baadhi ya changamoto zinazo mkabili ikiwemo uharibifu wa zao hilo
toka kwa Wanafunzi wa shule ya sekondari Mbosho.
Amesema kuwa
ikiwa serikali itapendekeza zao hilo kulimwa kwa wingi,yupo tayari kutoa miche
ya zao hilo ili wakulima waweze kuipata na kufaidi biashara yake iliyo na fedha
nyingi.
“Tusipende
kufanya kazi rahisi rahisi za kupata faida kwa haraka,ila tujenge utamaduni wa
kuwekeza kwa muda mrefu na kupata faida kwa muda mrefu kupitia zao hili,ambapo
kila familia na kizazi kijacho kita nufaika na zao hilo”alisema Paul.