June 20 hadi 22, 2017 Rais Magufuli alikuwa kwenye ziara ya kikazi siku tatu katika Mkoa wa Pwani ambako mbali na kuzungumza na wananchi wa Mkoa huo alizindua viwanda mbalimbali katika kuweka kwa vitendo kautli yake ya Tanzania ya viwanda.
Hapa nimekukusanyia mambo 15 miongoni mwa mambo mengi aliyozungumzia Rais JPM katika ziara hiyo ikiwemo issue ya usalama kwenye maeneo ya Kibiti, Mkuranga na Rufiji ambako kumekuwa na matukio ya mauaji ya raia na askari mfululizo, elimu, miundombinu na issue za ardhi na maji.
Hizi ni baadhi ya kauli zake>>>
1: Wataula wa chuya kwa uvivu wa kuchagua, nitawabana wezi wote ili tuondokane na usindikizaji wakati siye ni matajiri.
2: Kibiti na Rufiji hazina viwanda. Nani atakwenda kuwekeza huko wakati wanauana? Sisi ndio tunachelewesha maendeleo.
3: Mimi nachukia sana wezi; awe mwizi wa ndani au wa nje, mwizi ni mwizi tu. Wataula wa chuya awamu hii.
4: Kibiti nawaambia kwenye awamu hii hawatapita. Najua walikuwa wachache na moto wameshaanza kuuona. Narudia tena hawatapita.
5: Mkionana wachache wanalalamika mjue Magufuli anafanya kazi. Mkiona wachache wanalia wanasema Magufuli anatumbua semeni tumbua.
6: Kama Halmashauri haiwezi kujenga barabara waseme wasipewe fedha ili zibaki Serikali Kuu tujenge wenyewe barabara zetu.
7: Tumenunua ndege sita mpya hadi sasa. Zipo mbili zinazofanya kazi, nyingine inakuja na nyingine tatu zitakuja mwakani.
8: Kwa Taasisi zote hata kama ni Ofisi yangu ya Ikulu, kama hawatalipia maji suluhisho ni kukata.
9: wakati najiandaa kutoa hizi zawadi, ombi langu kwa wenye kiwanda mnapokabidhi hizi zawadi ninazofurahia sana muwe mnakabidhi zawadi kwa wafanyakazi wenu.
10: Kwa mfano, ungezungumza hapa umetayarisha hata Milioni Tano ambazo utawakabidhi wafanyakazi, mimi ningefurahi sana. Nawaombea Milioni Tano uwape wafanyakazi..? Basi kama atawapa Milioni Tano wafanyakazi mimi nitatelemka sasa kuwagawia na wengine.
11: Narudia tena, mimi katika kipindi changu mwanafunzi akipata mimba ndio kwa heri, hakuna kurudi shule.
12: Hata kama mimi mtoto wangu wa kike akipata mimba huko ataona kitakachotokea. Jamani Watanzania lazima niwambie ukweli.
13: Ipo siku mtakuta mwalimu anaingia darasa zima wanatoka kwenda kunyonyesha sababu huo mchezo ni mtamu kila mtu anaupenda.
14: Na Magereza nimeshawapa majukumu, tumechoka kuwalisha wafungwa. Mtu afungwe halafu Serikali itengeneze Bajeti ya kwenda kuwalisha wafungwa? Hii haiwezekani ndio maana nimetoa maagizo kwa Wakuu wa Magareza, wafungwa hawa wakalime ili waogope kufungwa.
15: Kwenye Wizara ya Afya tulitenga fedha mwaka juzi, zilikuwa Bilioni 31. Mwaka huu tumetenga Billion 250 na mwaka jana, za kununulia madawa. Wako radhi wakanunue madwa ya kutibu Maralia kuliko kununua madawa ya kuzuia Maralia.