WATU WASIOJULIKANA WACHOMA NYUMBA YA MWENYEKITI WA CCM WILAYA YA HAI


Mkuu wa Wilaya ya Hai Gelasius Byakanwa wa kwanza kulia akimjulia hali Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Hai Dkt Amini Uronu baada ya kunusurika kuteketea kwa moto huo.


Hai-Kilimanjaro.

WATU wasiofahamika wanatuhumiwa kuchoma nyumba ya Mwenyekiti wa Chama
cha Mapinduzi (CCM)wilaya ya Hai Dkt Amini  Uronu kwa kutumia  mafuta
ya gari ya aina  ya Petrol.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia  June 19 mwaka huu  majira  ya
saa  6 katika kijiji cha Nshara  kata ya Machame Mashariki  wilayani
hapa  wakati Mwenyekiti huyo akiwa amelala  na familia yake  ambapo
moto huo ulimjeruhi  mwenyekiti huyo sehemu za miguu na mikono.

Akisimulia tukio  hilo,mtoto wa Mwenyekiti Zahadi Uronu ulisema watu
wasijulikana walivamia nyumbani kwako na kuwasha moto milango  miwili
ambayo inatumikia kuingia na kutokea  kwa mafuta ya Petrol
"Tukiwa limelala tulushuka na kuona moto ukiwaka mlango wa nyuma
ambayo hutumika kwa ajili ya kwenda jioni na mlango wa mbele ambao
hutumika kwa ajili ya kuingia ndani" ulisema.

"Tulipiga kelele za kuomba msaada na ndipo watu walifika na kuvunja
mlango wa nyuma na hatimaye tulitoka wakati huo moto ulikuwa mkubwa na
tayari baba alikuwa amejeruhiwa miguu na mikono " alisisitiza
"Huu moto utakuwa umewashwa na watu kwani kwa upande wa nyuma ulianzia
mlango wa jikoni  na mlango wa mbele umeanza kuchoma vitu vilivyokuwa
kwenye baraza na milango  yote ndio kulikuwa chanzo cha moto.

Alifafanua kuwa siku ya tukio hilo kulikuwepo na wanafamilia nane
walikuwa wamelala katika nyumba hiyo ila kati ya hao ni baba yake tu
ndio aliyejeruhiwa na mama yake Arafa alipoteza fahamu kutokana na
mstuko wa tukio hilo.

Akizungumzia tikio hilo mmoja wa mashuhuda wa tukio  , Cuthbeth Uronu
alisema kuwa nyakati za usiku alistushwa na kilele zilisikika za
kuomba msaada ambapo  alifika na kukuta moto ukiwa unawake kwenye
milango
“Nilifika hapa nyakati za usiku nilikuta moto ukiwa unawake sehemu za
milango na niliamua kuvunja milango wa nyuma kwa kutumia gogo lilikuwa
hapo nje na ndipo hawa wanafamilia wakafamikiwa kutoka nje”alisema.

Akizungumza katika eneo la tukio hilo mkuu wa wilaya ya Hai, Gellasius
Byakanwa aliwataka wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili
kuwabaini wale wote waliohusika na tukio hilo
“Najua umeonyesha ushirikiano wa kutosha katika kunusuru maisha ya
familia hii naombeni hakikisheni kuwa ushirikiano huohuo mnatoa
kuwabaini waliohusika “alisema Byakanwa.

“ Naendelea  kufanya  uchunguzi zaidi wa  tukio hili nikibani kuwa
linahusiana na tukio la mwisho mwa wiki lilitokea katika kijiji hiki
na kuwapata waliohusika adhabu kali zitachukuliwa juu ya mtu
atakayebainika kuhusika na tukio hilo.

Kamanda wa polisi mkoani hapa , Selemani Issa alithibisha kutokea kwa
tukio hilo na kusema kuwa  mwenyekiti huyo amelazwa katika hospitali
ya St  Joseph ya mjini Moshi kwa ajili ya matibabu na uchunguzi zaidi
unaendelea kuwabaini waliohusika na tukio hilo.

Mnmo June 13 mwaka huu , kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya
iliondoa miundombinu ya maji katika shamba la Mbunge wa Hai, Freeman
Mbowe lililopo katika kijiji hicho kwa madai kuwa lipo kwenye chanzo

cha maji ya  mto Weruweru.