Hai-Kilimanjaro.
Wanafunzi wa shule za sekondari nchini wametakiwa kusoma kwa bidii
pamoja na kumcha Mungu ili waweze kufanikiwa katika masomo yao na kufanikisha
ndoto zao za kielimu kama vile vitabu vya dini vinavyo wataka kushika elimu.
Wito huo ulitolewa na
Diwani wa Kata ya Masama Mashariki mheshimiwa John Munis wakati
alipotembembelea shule mbili za sekondari zilizopo katika kata yake ambazo ni
Marire na Sawe na kuwapongeza waalimu
kwa kufundisha kwa bidii pamoja na wanafunzi waliofaulu vizuri katika masoma
mbalimbali.
Akikabidhi zawadi kwa wanafunzi hao mh Munisi alisema kuwa
anatambua jitihada zinazofanywa na waalimu hao katika kufanikisha ufaulu,na
kuwataka wanafunzi wote kuongeza bidii katika masomo na kuwaahidi kuwa
wanafunzi wote watakaofaulu kwa daraja la kwanza watapata zawadi bila kujali
wingi wao.
Alisema kuwa kila mmoja akitambua wajibu wake akiwemo mzazi,
mwalimu na mwanafunzi ufaulu utaongezeka
kwa asilimia kubwa na kusisitiza kila mmoja kutenda kwa haki .
Kwa upande wake diwani wa kata ya Machame Uroki Robsoni
Kimaro aliwapongeza waalimu wa shule
hizo kwa kufundisha kwa bidii bila kujali changamoto wanazokutana nazo huku akiwataka wanafuzi kuongeza bidii ya kusoma pamoja na
kuepuka matendo maovu ikiwepo ngono na
unywaji wa pombe.
Nae mwenyekiti wa bodi ya shule ya marire Dkt Abisai
Masawe na Mkuu wa shule hiyo mwalimu
Namkanda Kagonji amewashukuru madiwani hao kufika katika shule zao huku
wakihaidi kutekeleza mikakati yote waliyoipanga.