HAI-KILIMANJARO
Muda mfupi
kabla ya jina lake kutajwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara aliye kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Gelasius
Byakanwa ali wataka Wanafunzi wanao
tumia mfumo wa usomaji kwa njia ya
mtandao Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro kutumia vifaa hivyo kwa njia iliyo
kusudiwa ili kuweza kufikia lengo la utumizi wa vifaa hivyo Shuleni ili
kuendana na tekinolojia.
Rai hiyo
ilitolewa hapo jana wakati akizindua Tekinolojia ya usomaji kwa njia ya mtandao
katika shule ya sekondari ya Wasichana Machame,teknolojia iliyo wekwa na
mtandao wa Simu wa Tigo na kupewa jina la eschools.
Alisesema
kuwa wanafunzi hao wanatakiwa kuwa na mipaka ya usomaji kwa kutumia teknolojia
hiyo kwa kuzingatia masomo yalio wekwa ndani yake bila kutafuta ujuzi wa mambo
mengine ya utandawazi yasiyo kubalika.
“Siyo kila
kitu mnatakiwa kusimamiwa,itafika mahali utatakiwa kujisimamia wewe mwenyewe na
kusimamia wengine,sitegemei kusikia kuwa badala ya kutumia teknolojia hii ya
usomaji,muanze kuperuzi mambo yasiyo endana na kusudio hili.”alionya Byakanwa.
Kwa upande
wake Kaimu mkurugenzi wa Tigo kanda ya kaskazini Hendrick Nabo alisesema kuwa
Kampuni ya Tigo itazidi kusaidia serikali kuinua sekta ya elimu hapa nchini kwa
kuwezesha shule za sekondari na hata msingi kuendana na teknolojia.
“Tigo
inaelewa mahitaji ya wanafunzi katika maarifa ya Tehama,na inakutana na
mahitaji hayo kwa kutoa msaada wa mtandao kwa shule zilizo lengwa ili kutanua
ubunifu wao kwa kuwafanya Wanafunzi kujua dunia inaendaje.”alisema Nabo.
Kwa upande
wake Mkuu wa Shule hiyo Asteria massawe alimpongeza Mkuu wa Wilaya hiyo kwa
juhudi zake za kusikiliza na kutatua kero za shule wilayani Hai jambo ambalo
limeleta hamasa kwa wananfunzi na Waalimu.
Aidha
ameshukuru kampuni hiyo ya Tigo kwa kusadia uwepo wa tekinolojia hiyo shuleni
hapo,itakayo saidia kuwaandaa wanafunzi vizuri katika masuala ya Tehama wawapo
kazini au masomoni.
Mkuu wa Wilaya Gelasius Byakanwa pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Tigo Hendrick Nabo wakishangilia uzinduzi huo. |