Naibu Waziri wa TAMISEMI Mh.George Kakunda aliye simama akizungumza na Watumishi wa Halimashauri ya Wilaya ya Hai(kushoto) ni Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Hai Onesmo Buswelu na (kulia) ni mjumbe toka TAMISEMI. |
Naibu Waziri
wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI George Joseph Kakunda
amewataka Wazazi na Walezi Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro kuacha tabia ya kufumbia
macho watu wanaowapa ujauzito Watoto wa kike walio chini ya umri wa miaka kumi
na nane.
Kakunda
ameyasema hayo alipo kuwa katika ziara ya kutembelea miradi mbalimbali iliyo
fanywa kwa jitihada za wananchi na Serikali ikiwa ni pamoja na kuhamasisha
juhudi za maendeleo ili kutekeleza sera ya Tanzania ya Viwanda.
Amesema kuwa
hapo awali Mkoa wa Kilimanjaro ulikuwa ukisifika nchini kwa wazazi na walezi
kuwekeza katika sekta ya elimu kwa kuhakikisha Watoto wao wanakuwa wasomi, ila
kwa sasa mambo ya mebadilika kwa baadhi ya wazazi na walezi kujihusisha na
vitendo vya kuwapatia mimba watoto wa Kike walio chini ya umri wa miaka kumi na
nane jambo ambalo limekuwa ni aibu kwa Mkoa.
“Serikali
imejitahidi kubadilisha sheria kuanzia sheria ya elimu ya mwaka 1978 iliyo sema
kuwa mtoto wa kike akipata mimba afukuzwe shule,adhabu ya mtoto wa kike peke
yake huku aliye mpatia ujauzito akiachwa,Tumefanya mapitio makubwa mwaka 2002 Ya
sheria ya elimu bado iliendelea kutoa adhabu kwa mtoto wa kike peke yake tu.”alisema Kakunda.
Ameongeza
kuwa sheria ya makosa ya kujamiiana iliyo tungwa mwaka 1998 ilitoa nafuu kidogo
kwa mtoto wa kike kwa kutambua kuwa mtoto wa kike chini ya miaka 18 hata kama
akipelekwa nyumba za wageni kwa dhumuni la kufanya mapenzi naye kwa kukubaliana
au kuto kubaliana ni makosa ambapo kanuni ya adhabu ilifafanua vizuri adhabu
inayostahili kutolewa.
Kakunda
amesema kuwa mbali na sheria hizo kuwepo bado kuna watu wanacheza na sheria
hiyo kwa kumpatia Mtoto wa kike ujauzito au kufanya ubakaji ila Mahakamani
imekuwa ni tatizo kwa watu kuharibu ushahidi.
Akiongelea
adhabu ya sheria ya mwaka 2016 marekebisho ya sheria ya elimu,serikali iliweka
adhabu ya kifungo cha miaka 30 jela kwa mtu atakaye msababishia mwanafunzi
kupata ujauzito,au mtu aliye fanya njama kwa Mwanafunzi kuolewa lakini bado
ushahidi unaharibika na kufanya sheria hiyo kutokufanya kazi inavyo paswa.
Katika hatua
hiyo Waziri Kakunda amewataka viongozi wa kiserikali,dini na wananchi kukemea
wahalifu hao ikiwa ni pamoja ya kuwafichua wahusika na kutoshawishika kuharibu
ushahidi mahakamani ili haki iweze kutendeka.