Saa 24 baada ya taarifa hizo kupita mitandao ya Skysports na BBC SPORTS imeripoti na kumnukuu Adebayor kuhusu mpango wake wa sasa katika soka akiwa mchezaji huru, anasema bado ana mpango wa kurejea ligi kuu England na hajaizungumzia Yanga hata tone, hiyo imedhihirisha kuwa tetesi za kujiunga na Yanga sio za kweli.
“Nimepokea ofa chache kutoka timu za ligi kuu England na wote mnajua napenda kucheza England, licha ya kuwa mimi sio moja kati ya wachezaji wanaopendwa England nimecheza England kwa miaka kumi, ieleweke pia sikuja AFCON kucheza ili nipate timu nilikuja kuwakilisha taifa langu