Picha ikionesha madawa ya kulevya (picha kwa msaada wa mtandao) |
Picha ikionesha madawa ya kulevya (picha kwa msaada wa mtandao) |
Hai-Kilimanjaro
Waathirika
wa madawa ya kulevya wanaopambana kuachana nayo katika kituo cha Kilimanjaro
New Vison Sober House kilichopo Wilayani Hai mkoani Kilimanjaro,wame muomba Mkuu wa wilaya ya Hai Gelasius Byakanwa
kuwasaidia kutatua baadhi ya changamoto zinazo wakabili ili kuweza kukamilisha
ndoto zao za kuachana na matumizi ya
madawa ya kulevya.
Akizungumza
na Hai Kazi Blogspot Kiongozi wa
kituo hicho Haji Seleman Liyanga amesema kuwa ombi hilo kwa mkuu wa Wilaya ya
Hai limekuja baada ya changamoto kituoni hapo kuonekana kuwa kikwazo kwa waathirika
wa madawa ya kulevya, kushindwa kumudu hali iliyopo kwani waathirika
wanaopambana kuachana na madawa ya kulevya toka sehemu mbalimbali za Tanzania
imekua ikiongezeka kila mara kituoni hapo.
“Kiukweli
tuna kabiliwa na changamoto nyingi hapa kituoni mfano maji ni ya shida,vitanda ni
vichache,nyumba nayo ni ndogo huku idadi ya watu wanao tamani kuachana na
madawa ya kulevya wakizidi kuongekeza”alisema Liyanga.
Liyanga ameongeza
kuwa ikiwa changamoto hizo zitaweza kutatulika ,waathirika wa madawa ya kulevya
wanao fika kituoni hapo wataweza kubadilika kwa haraka na kurejea katika
shughuli za ujenzi wa Taifa,kutokana na mateso ya madawa hayo ya kulevya kuwa tesa
kwa kipindi cha muda mrefu.
“Unajua
mpaka mtu kufikia kuingia sober house ni dhahiri kuwa mateso makali aliyo
yapata anapambana kuondokana nayo,na ni vigumu mtumiaji wa madawa ya kulevya
kuacha na kurudia tena kutokana na madawa hayo yanavyo umiza mwili na
akili,hivyo ukiona mtu kaingia kupata huduma ya Sober House ni kwamba kajutia na yupo tayari kuacha”alisema
Liyanga.
Mbali na
kutoa ombi hilo kwa mkuu wa Wilaya Liyanga amewataka wadau mbalimbalia na
wanaharakati kusadia kutatua changamoto hizo kwa kizazi kinacho jutia utumiaji
wa madawa hayo ili kuweza kunusuru kizazi hicho na cha baadae.
Mbali na ombi hilo ameipongeza serikali kwa mkakati wake wa kuwafichua wauzaji na watumiaji wa madawa
ya kulevya,katika msako unaofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul
Makonda.