Afisa Elimu Msingi Agnes Luhavi akielezea Ubunifu ulio fanywa katika idara yao,katika shindano la Ubunifu lililo anzishwa na Mkuu wa wilaya ya Hai. |
Wafanyakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai wakifuatilia uwasilishwaji wa ubunifu katika idara zilizo kuwa zikishindanishwa |
Wafanyakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai wakifuatilia uwasilishwaji wa ubunifu katika idara zilizo kuwa zikishindanishwa |
Hai-Kilimanjaro.
MKUU wa
wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro Gelasius Byakanwa amezitaka idara zote za
Halmashauri ya wilaya ya Hai kuhakikisha kuwa wana kuwa wabunifu kiutendaji ili kuweza
kuhudumia jamii katika ubora unao hitajika na serikali.
Ameyasema
hayo jana wakatika wa muendelezo wa
shindano alilo lianzisha la
utoaji wa tuzo kwa idara inayo fanya vizuri kila mwisho wa mwezi ili kuweza
kuonesha ufanisi wa kazi zao kwa jamii wanayo ihudumia.
“Nipende
kuwa weka wazi kuwa kila idara inapaswa kushiriki kikamilifu katika shindano
hili ili kuweza kuacha kufanya kazi kwa
mazoe ya kukaa ofisini na kusubiri
taarifa toka nje,badala yake fanyeni kazi kwa kuifikia jamii ili kuweza
kudhibiti ukiukwaji unao weza kufanywa na watu mapema,na kwa kufanya hivyo
itakuwa ni rahisi katika utendaji wa idara husika.”alisema Byakanwa.
Katika
mashindano hayo yaliyo shirikisha idara tatu ikiwemo idara ya Elimu Msingi,Idara ya Elimu Sekondari na
Idara ya ujenzi na zima moto,washindi waliweza kupatikana ambapo idara ya
Ujenzi na zima moto iliweza kuibuka
mshindi na kukabidhiwa Kikombe cha ushindi.
Kwa upande
wake wa Mkandarasi toka Idara ya Ujenzi na zima moto Philipians Msangi ameeleza
kuwa jitihada za ubunifu zinazo fanywa na idara hiyo zimeweza kuzaa matunda na
kukubalika na wataalamu wengine ,ikiwa ni pamoja na kufanya kazi zilizo
shindikana kufanywa na wazabuni wa nje
kutokana na kiasi cha fedha kuwa kikubwa.
“Ukiangalia
wazabuni wa njee wanaopewa kazi mara nyingi wameonekana kushindwa kukamilisha
kwa wakati au kutumia fedha nyingi nabado kazi isionekane ila sisi tumeweza
kufanya na kuisidia Halmashauri yetu kupiga hatua.Alisema Msangi.