Mkuu wa Wilaya ya Hai Gelasius Gasper Byakanwa wa kwanza (Kulia) akimsikiliza Injinia wa Wilaya Cosmas Peace,aliye vaa kitambulisho,akiongea kwa vitendo,namna ujenzi wa barabara hiyo ulivyo kubalika kufanyika. |
Barabara ya Masama Mbweera ikionekana kuchimbwa asubuhi, mara baada ya Mkandarasi wa kampuni ya Mugenzo Company Ltd,kusikia Mkuu wa Wilaya hiyo anaitembelea. |
Hai-Kilimanjaro.
Mkuu wa
Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro,ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na
usalama Gelasius Byakanwa ametoa muda wa wiki mbili kwa kampuni ya ukandarasi ya MUGENZO COMPANY
LTD, kumaliza kazi alilyo pewa
ya ujenzi wa barabara ya Masama mbweera na barabara ya Kyeri machame Magharibi.
Ametoa agizo
hilo juzi wakati alipo tembelea barabara hizo mara baada ya kupokea taarifa
toka kwa wananchi kuwa ujenzi unao fanywa na Mkandarasi huyo upo chini ya
kiwango, mbali na muda alio pewa wa miezi mitatu toka mwaka jana 2016 kuto
kukamilika.
“Hatuwezi
kuona pesa za serikali zinatumika kumbe zina tumika chini ya kiwango,ni agize
ya kuwa Mkandarasi huyu akishindwa kukamilisha barabara hizi asilipwe kiasi
chochote ili iwe fundisho kwa Wakandarasi wengine wanao tumia pesa vibaya na
kuchelewesha shughuli za kuhudumia wananchi”alisema Byakanwa.
Akitoa
ufafanuzi wa ujenzi wa barabara hizo Mhandisi wa barabara Wilaya ya Hai Injinia
Cosmas Peace amesema kuwa mkandarasi alipewa tenda hiyo toka mwaka jana
akitegemewa kuikamilisha mwezi wa kumi na moja mwaka jana,badala yake
alishindwa kufanya hivyo kwasababu zisizo weza kujulikana.
Amesema kuwa
ujenzi wa barabara ya Masama Mbweera ulikuwa ni wa kilomita tatu,kwa kiwango
cha kushindilia changarawe na barabara ya kyeri kilomita mbili kwa kiwango
hicho hicho zote zikiwa na jumla ya shilingi milioni sitini na tano,fedha
zilizo toka katika mfuko wa barabara,ambapo mpaka sasa Mkandarasi huyo amesha
lipwa shilingi milioni ishirini na mbili laki moja na elfu thelathini.
Katika hatua
hiyo Byakanwa amewataka viongozi wa serikali za mtaa kusimamia na kutoa taarifa
za kila aina ya ujenzi unaofanyika katika maeneo yao ili kuweza kuwa na
miundombinu iliyo kidhi vigezo vinavyo hitajika na Serikali.
“Nasikitika
kusikia kuwa Mkandarasi huyu alikuwa kimya pasipo kuendeleza ujenzi huu mpaka
pale alipo sikia kuwa nakuja kutembelea barabara hizi ndipo alipo anza kuchimba
barabara”Alisema Byakanwa.