Mkuu wa Wilaya Gelasius Byakanwa wa tatu (kushoto),Mkurugenzi wa Halimashauri ya wilaya Yohana Sintoo wa pili toka upande wa (kulia) wakifurahia mchango wa Mabati toka benki ya CRDB tawi la Hai.
Hai-Kilimanjaro.
Mkuu wa Wilaya ya Hai Gelasius Gasper Byakanwa amesema kuwa serikali ya wilaya imejipanga
kupoboresha hali ya mazingira ya shule ili wanafunzi waweze kupata elimu katika
mazingira bora na safi.
Byakanwa alitoa kauli hiyo wakati akikabidhi Mbao Katika Shule Za Msingi Wilayani Hai Kwaajili ya ujenzi wa Vyumba Vya Madarasa ili kuondoa msongamamo wa wanafunzi madarasani pindi vyumba hivyo vitakapokamilika.
Alisema shule zitakazonufaika na mbao hizo ni zile ambazo
tayari zimeanza ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa kupitia nguvu za wananchi
pamoja na serikali kuunga mkono jitihada zao kwa kuwapatia mbao za kupaulia
pamoja na mabati.
Alizitaja shule zilizonufaika na mgao wa mbao hizo ni Bomani, Gezaulole na Msamadi, ambapo kila shule
ilipatiwa mbao 160 zilizokabidhiwa Kwa
Kamati ya Shule hizo, Amezitaka Kamati hizo kusimamia Ujenzi Wa Madarasa Mpaka
Utakapo Kamilika katika kiwango kinacho hitajika.
“Nataka kuona watoto wetu wakipata elimu iliyo kamilika,tena
katika mazingira ambayo ni rafiki kwao,ili ibaki kazi moja tuu ya wao
kuzingatia masomo na kufaulu”alisema Byakanwa.
Aidha Meneja Wa Benki Ya CRDB
Tawi la Hai Philimon Pindapinda Amemuunga
Mkono Mkuu huyo Wa Wilaya Kwa Kukabidhi Mabati 115 Kwa Shule Ya Msingi Bomani
Ikiwa Kama Mchango Wa Benki Hiyo.
Naye Diwani wa Kata ya Bomani Joely Nkya Ametoa Shukrani Kwa
Mkuu Wa Wilaya Hiyo Kutokana na Kufanya kazi Inayoleta Maendeleo kwa
kuwashirikisha wadau mbalimbali pasipo kujali itikadi ya vyama jambo linalo
pelekea Wilaya ya Hai kukua kwa sasa.
|