|
Wa katikati pichani ni Mkuu wa Wilaya ya Hai Gelasius Byakanwa, kushoto kwake ni Mkuu Wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Meck Sadick na kulia kwake ni Mwekezaji Trevor G.Fford |
|
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Meck Sadick akiongea na wafanyakazi wa shamba la ushirika la Masama Roo wakati wa utambulisho wa Mwekezaji huyo. |
|
Jensen Natai Meneja wa Shamba hilo aliye vaa shati la drafti akimtambulisha mwekezaji Trevor Fford kwa wafanyakazi wa shamba hilo.
Hai-Kilimanjaro
MKUU wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Meck Sadick amewataka wafanyakazi wanao fanya kazi katika mashamba ya wawekezaji kuacha kuwavuruga wawekezaji badala yake kuwaacha wafanye kazi kulingana na mikataba waliyo ingia.
Ameyasema hayo Jana wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro Kata ya Masama roo wakati alipotembelea shamba la kahawa ambalo linasimamiwa na vyama vya ushirika kwa lengo la kumuona mwekezaji mpya atakaye wekeza katika shamba hilo.
Sadick amesema kuwa tabia ya baadhi ya wafanyakazi kuvuruga utaratibu wa mwekezaji aliopewa wakati wa kujaza mkataba wake umekuwa ukiathiri shughuli za uwekezaji na kuleta usumbufu ambao unaweza pelekea wawekezaji kushindwa kuwekeza.
“Ifike mahali sisi wananchi tueshimu maagizo na mkataba anao pewa m wekezaji ili stahiki zetu tuweze kuzipata kwa wakati,tukishindwa kufanya hivyo na badala yake tuka walete vurugu au usumbufu wowote ni wazi kuwa watashindwa kufanya shughuli iliyo waleta na kuondoka huku tukibaki katika umasikini na kushindwa kuji kwamua”alisema Sadick.
Kwa upande wake Mkuu Wilaya ya hiyo Gelasius Gasper Byakanwa alimtaka meneja wa shamba hilo kuhakikisha utelekezaji wa mwekezaji huyo unafuata taratibu za mkataba ili kuepusha mgogoro na wafanyakazi kama ilivyo kuwa hapo awali.
“Hakikisha unakaa na mwekezaji ili kuweza kufanya utaratibu utakao ridhisha wafanyakazi pamoja na ofisi yangu ikiwa ni pamoja na kuweka mikakati iliyo bora ya kuisaidia jamii iliyo wazunguka kutatua baadhi ya changamoto zinazo wakabili,ili uwekezaji uwe wa faida.”alisema Byakanwa.
Naye Mwekezaji huyo Trevor G Fford amewataka wafanyakazi wa mashamba hayo kuwa wawajibikaji katika shughuli zitakazo kuwa zina wahusu ili kuweza kunusuru hali ya shamba,kutokana na shamba hilo kuonekana kukosa matunzo mazuri kwa uzalishaji.
“Niwashukuru kwa kunikaribisha,nipende kuwaomba kuwa inatupasa kufanya kazi kwa bii ikiwa ni pamoja na kuepuka wizi,rushwa,uvivu na uongo eneo la kazi ili kuweza kupiga hatua kwa haraka na kupata manufaa mazuri”alisema Fford.
|
Chama hicho
cha ushirika wa Masama Roo ni muunganiko
wa vyama vingine vitatu ikiwemo Mudio,Sawe na Sonu ambapo shamba lililo pewa
mwekezaji lina ukubwa wa hekari 254.