Mkuu wa Wilaya ya Hai Gelasius Byakanwa na Mkurugenzi wa halmashauri wakiongoza mbio za mazoezi,wakifanikiwa kuwa wa kwanza kwa kituo cha kwanza kabla ya kurudi uwanjani. Hai-Kilimanjaro |
Wananchi Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro wametakiwa kuzingatia kufanya mazoezi ili kuweza kujenga afya zao na kuepeukana na magonjwa yasiyo kuwa ya lazima kwa kutokufanya mazoezi.
Hayo
yamesema na Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi ambaye ni Mkuu wa Wilaya hiyo Gelasius Byakanwa akiwa
mgeni rasmi katika uzinduzi wa utekelezaji wa agizo la Makamu wa Raisi Samia Suluhu
Hassan kufanya mazoezi kila jumamosi ya pili ya mwezi.
Amesema kuwa
Wilaya hiyo imeongeza siku ya kufanya mazoezi badala ya kufanya mazoezi kwa
jumamosi moja na kuwa mazoezi yatakuwa ya jumamosi mbili kila mwezi.
“Kwa
kutambua umuhimu wa kufanya mazoezi tumeona Wilaya yetu ifanye mazoezi kwa Jumamosi
mbili ndani ya mwezi mmoja ili kujenga miili yetu,nina shukuru kwa kuwa wito
huu wa kufanya mazoezi umepokelewa vizuri na wananchi wetu”alisema Byakanwa.
Kwa upande
wake Mwenyekiti wa kamati hiyo ya maandalizi ya mazoezi Katibu Tawala Wilaya ya
Hai Upendo Wella,amewapongeza wananchi kwa kujitokeza katika zoezi la kufanya
mazoezi pamoja na wananchi kukubali mazoezi hayo kuwa mara mbili.
“Najivunia
kuona mwitikio umekuwa mkubwa katika zoezi hili la kufanya mazoezi pamoja na
kupima magonjwa kama Shinikizo la damu,VVU UKIMWI sambamba na uchangiaji wa
damu,ni wazi kuwa kila mmoja ameona umuhimu huu na kufurahia kuona kwamba ameweza
kukimbia na kupata mafunzo ya njia sahihi ya kufanya mazoezi”alisema Wella.
Katika
uzinduzi huo wa kufanya mazoezi,pia washiriki walipata nafasi ya kupia afya zao
kwa hiyari ikiwa ni pamoja na kuchangia damu salama kwa watu wenye uhitaji
ikiwemo akina mama walio jifungua,Watoto wadogo pamoja na majeruhi wa ajali
ambao wanaweza kusaidiwa na damu hiyo.
Mazeoezi yakiendelea leo asubuhi kuelekea uwanja wa Jimbo kwa mazoezi zaidi.
|
Wadau wa mazoezi wakijipanga kuungana na wenzao katika mazoezi |
Wadau wa mazoezi wakifurahia mbio zao kabla ya kuingia uwanjani. |
Afisa elimu Sekondari Wilaya ya Hai Julius Kakyama aliye vaa nguo za bluu akifuatilia maelekezo ya njia sahihi ya kufanya mazoezi. |
Waongozaji wa mazoezi wakielekeza washiriki njia za kufanya mazoezi uwanja wa jimbo. |
Mazoezi yakiendelea kila mmoja akijitahidi kuonesha umahiri wake pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Hai. |
Mazoezi yakiendelea kila mmoja akijitahidi kuonesha umahiri wake. |
Mazoezi yakiendelea kila mmoja akijitahidi kuonesha umahiri wake. |
Watumishi wa Idara ya Afya hosipitali ya Wilaya ya Hai wakifuatilia michezo uwanjani. |
Katibu Tawala Wilaya ya Hai ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya mazoezi Upendo Wella akisalimiana na wachezaji wa mpira wa miguu. |
Wachezaji wa mpra wa kikapu wakionesha uwezo wao katika siku ya mazoezi. |
Mkuu wa Wilaya ya Hai Gelasius Byakanwa akishiriki zoezi la kupima afya na kuchangia damu. |