Hai-Kilimanjaro.
Mahakama ya Wilaya ya Hai Mkoa
wa Kilimanjaro imemuhukumu mwanafunzi mmoja wa kidato cha tatu wa Shule ya Sekondari,
mwenye umri wa miaka 16 mkazi wa Kikavu chini adhabu ya kuchapwa kiboko kimoja kwa
kosa la kumbaka mwanafunzi mwenzake na kumpa ujauzito.
Adhabu hiyo ilitolewa juzi
na Hakimu mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo Agness
Mhina baada ya kuridhishwa na ushahidi ulio tolewa mahakamani hapo na mashahidi sita wa upande wa mashtaka.
Akisoma hati ya mashtaka
Mahakamani hapo mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo Valeria Banda, alisema
kuwa mshitakiwa alifanya kosa hilo siku isiyojulikana mwezi wa oktoba mwaka
2015 maeneo ya Mkalama Wilaya ya Hai ambapo alimbaka mwanafunzi mwenzake
wakidato cha tatu na kumpa ujauzito.
Kabla ya hukumu hiyo kutolewa
Mwendesha mashitaka Valeria Banda, alidai kuwa vitendo na matukio ya ubakaji
yamekuwa yaki tendeka katika jamii,huku jamii ikiwa na uelewa wa kufanya
matukio na vitendo hivyo ni kinyume na sheria.
Walio toa ushahidi katika
kesi hiyo ni pamoja na Daktari wa hosipitali ya Wilaya ya HAI,Ofisa wa jeshi la
Polisi kutoka dawati la jinsi,wanawake na watoto,Mama mzazi wa Mwanafunzi
huyo,Mwalimu wa shule anayosoma pamoja
na aliye pata ujauzito.
Aidha Mahakama imetumia sheria ya alama ya adhabu kutoa hukumu hiyo
huku kesi hiyo ikisimamiwa kupitia kifungu cha elimu namba 5 cha sheria ya elimu
namba 25 ya mwaka 1978 iliyosomwa, pamoja na gazeti la serikali namba 265 ya
tarehe 5 ya mwezi 9 mwaka 2003.