UFUGAJI WA MBWA KIHOLELA WAWAPA KERO BAADHI YA WANANCHI HAI.



Hai-Kilimanjaro


Wakazi wa Bomang'ombe Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro,wamelalamikia vitendo vya baadhi ya Watu kujiusisha na ufugaji holela wa mbwa ambao umesababisha usumbufu mkubwa kwa wananchi.

Wakizungumza na Haikaziblog kwa nyakati tofauti,wananchi hao wamelalamika kwa kushindwa kuwadhibiti na kusababisha wanyama hao kuzuruza ovyo na kugeuka kero kubwa.

Mmoja wa Wananchi hao Juma Saidi Mkazi wa Mtaa wa Bomani,alisema kuwa ustaarabu umeanza kutoweka katika eneo hilo kutokana na mbwa hao kuzurula ovyo huku wengine wakivamia nyumba za watu ili kujipatia lishe

Alisema wananchi wameshindwa kujua mtu atakaye waondolea kero hiyo kutokana na uongozi wa serikali  katika eneo hilo kukaa kimya bila ya kuwasiliana na wamiliki wa mbwa hao.

'' licha ya kukosekana kwa ustaarabu kutokana na wanyama hao kuingia kwenye makazi lakini pia kuna uezekano mkubwa wakasababisha magonjwa kwa binadamu ''alisema Saidi.

Joseph Macha mkazi wa Kibaoni alisema anafahamu mbwa  wenye magonjwa wanaleta maambukizi kwa binaadamu akitaja ugonjwa wa kichaa cha mbwa'rabies' na iwapo atamung'ata binadamu atapata ugonjwa

Hawa mbwa wamekuwa wakila mifugo ikiwamo kuku wanalamba vyombo wakikuta vikiwa  nje hivyo tunaomba idara ya mifugo kuchukua hatua za haraka  kwa wamiliki wa mbwa ili wadhibiti wanyama wao.

Elia  Machange, Asifa mifugo wa Halmashauri hiyo,alisema tatizola mbwa kuzurula ovyo hapa mjini ni kubwa na hata wakati mwingine kutishia wanafunzi wanao kwenda shule nyakati za asubuhi,tunachukua hatua muda sio mrefu tutatumia risasi na hata sumu kuwamaliza hawa mbwa wanaodhurula ovyo ili kmaliza tatizo hili.