Mkuu wa Wilaya ya Hai Gelasius Gasper Byakanwa akisalimiana na mtoto kutoka kaya inayo nufaika na ruzuku toka TASAF,Kijiji cha Rundugai alipo watembelea. |
Mkuu wa Wilaya ya Hai Gelasius Gasper Byakanwa akioneshwa sehemu ambayo mnufaikaji wa ruzuku toka TASAF,hulala pamoja na familia yake. |
Mkuu wa Wilaya ya Hai akizungumza na kaya 91 za watu wanao nufaika na ruzuku toka TASAF,akiwahimiza kukata bima ya afya ili kumudu gharama za matibabu. |
Walengwa wa ruzuku toka TASAF wakimsikiliza Mkuu wa wilaya. |
Hai-Kilimanjaro.
WANANCHI wanao
nufaika na mpango wa kunusuru kaya masikini Wilayani Hai Mkoani
Kilimanjaro,wametakiwa kuhakikisha wanatumia fedha wanazopata kukata bima ya
afya pamoja na kugawa katika matumizi mengine muhimua na msingi ili kuweza
kujikwamua kiuchumi.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Hai Gelasius Gasper
Byakanwa wakati alipokuwa akitembelea kaya hizo ili kuhakikisha ikiwa fedha zinazo
tolewa na TASAF zinawafikia walengwa kwa wakati na kutumika katika matumizi
sahihi.
Amesema kuwa Mratibu
wa TASAF wilaya anapaswa kuhamasisha zoezi la kila kaya kukata bima ya afya ili
kuweza kusaidia gharama za matibabu kwa kaya hizo,kwani suala la matibabu
limekuwa changamoto kwa walio wengi kushindwa kumudu fedha za matibabu kutokana
na kukosa bima ya afya.
Byakanwa ameongeza kuwa kila kaya inayo nufaika na ruzuku
hiyo kutoka TASAF zinapaswa kubuni miradi midogomidogo kama vile ufugaji wa
kuku,mbuzi, kondoo na bustani za mbogamboga ili kuweza kuzalisha mali itakayo
wasaidia kutatua matatizo yao ikiwa mpango huo utafikia tamati,jambo litakalo
kuwa lime wajengea uwezo wa kujitegemea.
"Mpaka mwezi wa saba nitakapo kuja tena kuwatembelea nitafurahi kuona kila kaya ina bima ya afya,itakayo wasaidia kupata huduma za matibabu"alisema Byakanwa.
Kwa upande wake Mratibu wa TASAF Wilaya ya Hai Eric
Marichamu amesema kuwa, wamepokea fedha za kaya masikini sh 126.4 milioni
zitakazo nufaisha vijiji 43 vyenye kaya 3,778 zilizo dhibitishwa kuingia katika
mpango huo.