Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai,(katikati) ni Mkuu wa Wilaya ya Hai Gelasius Byakanwa na wa mwisho (kulia) ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai. |
Mkuu wa wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro Gelasius Gasper
Byakanwa amewataka Madiwani katika Halmashauri ya Wilaya ya hiyo kufanya kazi
kwa Uangalifu na kwakushirikiana ili kuleta maendeleo wilayani hapo.
Ameyasema hayo katika
ufunguzi wa semina ya siku mbili kwa madiwani wa halmashauri ya wilaya
iliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya Ya Hai ambapo amewataka
Madiwani kuwa vipaumbele na kuhakikisha miradi inayoanzishwa kwenye jamii iwe
imenzishwa na wananchi wenyewe ili kuiwezesha jamii kuwa na uwezo wakujitegemea
kwaajili ya maendeleo yao.
Byakanwa ameongeza kuwa
maendeleo katika jamii hayangalii itikadi za chama hvyo ni wajibu kwakila
kiongozi hususa ni madiwani hao kushurikiana na jamii kuainisha miradi ambayo
tayari imefikia hatua inayostaili kupewa fedha, na kusisitiza kupewa taarifa ya
mtu yoyote ambae anakwamisha miradi hiyo
bila kumuonea mtu wala kujali kuwa anatoka chama gani.
Nae mwenyewkiti wa
Halmashauri ya Wilaya ya Hai Bi.Helga Mchovu amemshukuru mkuu wa Wilaya kwa
juhudi zake za kushirikiana na Madiwani hao katika mambo mbalimbali hususa
kuleta maendeleo kwa wananchi na Halmashauri kwa ujumla,huku akiwataka madiwani
kufanya kazi na kushirikiana na wananchi katika kuleta maendeleo katika jamii.
"Nipende kukupongeza Mkuu Wetu wa Wilaya pamoja na Mkurugenzi kwa kazi nzuri munazo fanya ikiwa ni pamoja na njia munazo fanya ya kushirikiana na sisi Madiwani katika nafasi ya kuleta maendeleo kwa wilaya yetu,nafurahi kwakuwa hatuna uchama katika shughuli za maendeleo"alisema Mchomvu.