![]() |
Picha ikionesha uharibifu wa mazingira unaofanywa na wakazi wa Wilaya ya Hai Kata ya masama kati na Masama Mashariki katika mto Namwi ulio tegemezi kwa wakazi waishio tambarare |
![]() |
Wananchi waliojitokeza kupanda miti katika mto Namwi wakimsikiliza Diwani wa Kata ya Masama Kati,wakati akiwapongeza kwa zoezi hilo muhimu la kunusuru mazingira. |
![]() |
Picha ikionesha bonde la mto Namwi na miti iliyo pandwa na wananchi. Hai-Kilimanjaro |
CHANZO cha uharibifu wa mazingira katika mto Nawi uliopo katika kijiji
cha Nguni Wilayani Hai mkoani Kilimanjaro imeelezwa kuchangia
kukosekana kwa maji katika maeneo ya
ukanda wa tambarare katika
wilaya hiyo.
Uharibifu huo ambao umefanywa na baadhi ya wananchi kwa kufanya
shughuli za kinadamu bila kujali
madhara ya shughuli wanazozifanya
kumepelekea wananchi kukosa maji kwa ajili ya matumizi ya nyumbani
pamoja na kukwamisha kilimo cha
umwagiliaji .
Akizungumza katika zoezi la upandaji miti katika mto huo , diwani wa
kata ya Masama kati Deogratius Kimaro
alisema shughuli za kibidamu
zinazofanywa katika mto huo unaotegemewa kupelekea maji kwa wananchi
wanaoishi ukanda wa tambarare na
kukosa maji hali ambayo imepelekea
kupungua kwa maji na kushindwa
kufanya shughuli nyingine za
uzalishaji.
“Ndugu wananchi shughuli mnazofanya katika mto huo zimesabisha madhara
makubwa kwa wakazi wa ukanda wa tambarare na hata sisi wa ukanda huu
kwani maji ni machache kwenye mto
huu kutokana na sisi mwenyewe
kulima kwenye vyanzo pamoja na kukata miti ambayo ilisaidia kuboresha
uoto wa asili” alisema Kimaro.
Alisema , jukumu la utunzaji wa mazingira ni la kila mmoja na kuondoa
dhana iliyojengeka miongoni mwa baadhi ya jamii kuona kuwa zoezi la
utunzaji wa mazingira ni la serikali
kitu ambacho si sahihi na
kuwataka kuondokana na dhana hiyo.
Nae mkazi wa kijiji hicho Onesmo
Kileo alisema kuwa shughuli za
kibinadamu zinaendelea katika vyanzo vya maji kutokana na dhana
iliyojengeka kwenye jamii kuwa maeneo hayo ni ya urithi na
wanayamiliki kihali na kuamua kufanya shughuli hizo.
Kwa upande wake ofisa misitu wa kata, Masama Mashariki John Katikirwa
, alisema wanakabiliana changamoto kubwa katika zoezi la kudhibiti
hali ya uharibifu wa mazingira kutokana na baadhi ya viongozi
kushirikiana na watu wanaohusika na uharibifu mazingira.
Hata hivyo Katikirwa alisema zoezi la upandaji wa miti litakuwa
endelevu kwa lengo la kurudisha hali ya uoto wa asili uliopotea
kutokana na baadhi ya watu kukata , kulima
na kuchoma miti katika
maeneo yalitengwa kwa ajili ya utunzaji wa mazingira