Hai-Kilimanjaro.
Wanaume
Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro wametakiwa kuwashirikisha wenza wao katika
biashara wanazo endesha pamoja na kuwa
ruhusu kufanya kazi walizo somea au kujiajiri ili kupunguza makali ya maisha
pindi mwanaume atakapo fariki na kumuacha mwanamke katika hali ya ujane.
Rai hiyo
imetolewa na akina mama wajane wa Wilaya ya Hai wakati wa maadhimisho ya siku
ya wajane duniani iliyo wakutanisha wanawake wajane toka maeneo mbalimbalil ya
wilaya hiyo wakiongozwa na kauli mbiu ‘WAJANE WANAMCHANGO MKUBWA KUELEKEA TANZANIA
YA VIWANDA”.
Kwa upande
wake Anande Onesmo Salema ambaye ni mjane amesema kuwa changamoto zinazo
wakumba wanawake wajene mara baada ya kufiwa ni pamoja na baadhi ya wanaukoo
kuwarithisha kwa wanaume wengine ndani ya ukoo,kunyang’anywa mali zilizo
achwa,kufukuzwa pamoja na kunyang’anywa
watoto.
Amesema kuwa
kitendo cha kurithisha mwanamke kwa mtu mwingine kimekuwa kikiwaumiza wajane
kutokana na kukosa huduma stahiki zilizo kuwa zikitolewa na mume ambapo mrithi
amekuwa akishindwa kutoa huduma hizo ipasavyo.
“ni ukweli
kuwa mrithi hawezi kutoa msaada wa ukamilifu kwakuwa baadhi ya huduma
alizotakiwa kuziotoa kwa mjane huzipeleka kwa mke wake hivyo hali hiyo niya
uonevu na unyonyaji zaidi ulio kithiri vijijini.”alisema Salema.
Kwa upande
wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Hai Helga Mchomvu amesema kuwa
tabia ya baadhi ya wanaume kuwakataza wanawake kufanya kazi au biashara ya
kutafuta kipato cha familia ni kitendo kisicho kubalika kwani huleta madhara
makubwa wakati mwanaume atafariki kuiacha familia katika wakati mgumu,kwani
Mwanamke haja zoea kutafuta.
“inashangaza
kwa kweli baadhi ya wanaume kuwa kataza wanawake wao kufanya kazi,unakuta
mwanaume amekuwa katili katika suala hilo pasipo kujua kuwa ipo siku anaweza
kufariki na kumuacha mke na watoto katika mazingira ya kuwa tegemezi”alisema
mchomvu.
Akisoma risala
ya wanawake wajane mbele ya Mgeni rasmi Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Yohana
Sintoo Mama Shangali amesema kuwa Umoja wa Mataifa unatambua kuwa mamilioni ya
wajane ulimwenguni kote wanateseka na matatizo makubwa yanayo sukumwa na jamii
wanayo ishi ikiwemo unyanyasaji wa
kingono, umaskini wa kiuchumi ulio kithiri,utapia mlo kwa watoto wao na watoto
kukosa elimu bora na malazi.
Ameongeza
kkuwa mali ambazo mjane amechuma na mume wake zimekuwa zikichukuliwa kinguvu na
ndugu wa mume na kuacha familia nyingi zikiishi katika hali ya ukiwa.
Kwa upande
wake Mratibu wa maadhimisho hayo kiwilaya mwanaharakati Mese Ndosi ameiomba
serikali kuwasaidia wajane katika masuala ya kisheria pindi wanapo dhulumiwa
mali zao ili kuweza kuzirudisha mikononi mwao.
“Tunaiomba
serikali itusaidie na iwasaidie wajane kwa kuwapa wanasheria wakati wa kesi zao
mahakamani ili waweze kupata haki zao stahiki na kuwafanya kuto kujutia hali ya
ujane walio nayo”alisema Ndosi.
Amesema kuwa Siku ya kimataifa ya wajane ilibuniwa mwaka 2005
kupitia usaidizi wa wakfu wa Loomba na kutambuliwa rasmi na Umoja wa Mataifa
mnamo mwaka 2010.
Wakfu wa Loomba ulibuniwa
mwaka 1997 na Lord Raj Loomba kama njia ya kumkumba mamake ambaye alibaki mjane
akiwa na umri wa miaka 37 eneo la Punjab nchini India.
“Aliongeza
kuwa Wakfu huo unalenga kuwaelimisha watoto wa waajane maskini na kuwainua
wajane kote duniani. Tangu kubuniwa kwa siku ya wajane duniani mwaka 2005 wakfu
huo umewaelimisha maelfu ya watoto wa wajane maskini na kuwasaidia zaidi ya
watu 27,000 wa familia zao”aliongeza Ndosi.