MOSHI
IMEELEZWA
kuwa jitihada za sasa za Serikali kuboresha miundombinu ya usafirishaji na kupeleka nishati ya umeme vijijini
vitapunguza changamoto na kuongeza fursa za viwanda kupitia Ushirika.
Hayo
yameelezwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika Profesa Faustine Karrani
Bee katika ufunguzi wa warsha ya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi na Wanahabari
kuhusu elimu ya Ushirika Nchini na mchango wa Chuo katika kuendeleza ushirika.
Amesema kuwa
Ushirika ndio njia pekee ya usawa ya kujenga uchumi utakao milikiwa na
watanzania ambapo uchumi utamuondoa Mtanzania katika umaskini na kumuwezesha
kumiliki rasilimali za nchi.
Bee amesema
kuwa Tafiti,elimu na ushauri vinavyotolewa na chuo cha Ushirika Moshi
vinahitaji na vimekuwa vikipata ushirikiano wa karibu kutoka kwa wanahabari ili
kufikia malengo yanayo tarajiwa ya jamii kuwa na uelewa na kuzidi kuviamini
vyama vya ushirika nchini.
Chuo kikuu
cha Ushirika kitazamia mtazamo chanya kwa watanzania katika kufikia malengo ya
ushirika hapa nchini,kwa kushirikisha wadau mbalimbali katika kutoa elimu ya
Ushirika na kuhakikisha kuwa jamii inapata habari sahihi za Ushirika.
Ameongeza
kuwa kwa sasa vyama vingi vya ushirika vimekuwa na changamoto mbalimbali zilizo
pelekea uaminifu wa vyama vya ushirika kutoweka katika jamii,hivyo kumtaka
Mrajisi wa vyama vya Ushirika kufanya jitihada za kurudisha imani hiyo kwa
wananchi kwa kutoa maelekezo kwa vyama vya msingi vya ushirika nchini.
Kwa upande
wa Wanahabari katika Warsha hiyo wametaka Chuo kikuu cha Ushirika ambacho ndio
watendaji wakuu wa Elimu ya Ushirika
nchini kuondoa dhana ya kupenda kuongelewa kwa mazuri kwani wengi hawapendi
kukosolewa na ndio chanzo cha kuwa mbali na wanahabari.
Aidha
wamebainisha kuwa vyombo vya habari vimekuwa vikishutumiwa kwamba vinaleta
uchochezi pale vinapo tafuta na kutoa taarifa kuhusu ubadhirifu na madhaifu
mengine ya ushirika jambo ambalo ni kinyume
hivyo kutaka Chuo hicho kutoa elimu kwa jamii na watendaji wa bodi za
vyama vya ushirika kukubali kazi za wanahabari.
Warsha hiyo
imelenga kuanzisha na kuendeleza ushirikiano wa pamoja kati ya chuo kikuu cha
Ushirika Moshi- MOCU na Wanahabari katika kutekeleza mpango wa kuendeleza Elimu
ya Ushirika hapa nchini pamoja na kutoa fursa kwa wanahabari kufahamu shughuli
mbalimbali zinazofanywa na chuo katika kutoa elimu ya ushirika.