HAI-KILIMANJARO
Imebainika
kuwa baadhi ya wanawake wanao jifungua wanashindwa kunyonyesha watoto wao
ipasavyo kutokana na kuwa na msongo wa
mawazo unao sababishwa na akina Baba.
Hayo
yamebainishwa na Dr Jane Mcharo Mratibu
wa Afya ya uzazi na Mtoto toka hosipitali ya Wilaya ya Hai alipo kuwa
akizungumza na kituo hiki ofisini kwake kwa lengo la kujua umuhimu wa Wanaume
wakati wa Mwanamke akinyonyesha.
Amesema kuwa
Mwanaume ana mchango mkubwa sana kwa Mke wake hivyo kuhitajika kuhudhuria
kliniki na Mke wake kipindi cha ujauzito
ili kuweza kupata elimu ya uzazi ya kumtunza mke na Mtoto.
Mcharo
ameongeza kuwa wanaume wanahitajika kutumikia nafasi zao ipasavyo ikiwa ni
pamoja na matunzo kwa Mama na Mtoto kwa kuwa nao karibu,huku akihakikisha kuwa
mama na mtoto wanapaswa kula vizuri,kulala na kuvaa vizuri ikiwa ni moja ya
nguzo muhimu ya jukumu lake.
Amebainisha
kuwa Wanawake wamekuwa wakipata tatizo la kutokuweza kunyonyesha ipasavyo
kutokana na msongo wa mawazo wanao pata toka kwa Mwanume ikiwa ni pamoja na
baadhi ya Wanaume kutoka nje ya ndoa na kushindwa kutimiza majukumu yake ya
kuleta chakula na mahitaji muhimu nyumbani.