Serikali Wilayani
Hai Mkoani Kilimanjaro imepongeza Benki ya NMB Tanzania kwa kuamua kuisaidia
shule ya sekondari maili Sita kuwa sehemu ya shule iliyo pokea kompyuta saba
kwaajili ya kukuza teknolojia ya mawasiliano shuleni.
Pongezi hizo
zimetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Hai Gelasius Byakanwa wakati akipokea kopyuta
saba toka kwa Mkurugenzi wa Benki ya NMB Tanzania Bi.Ineke Bussemaker.
Amesema kuwa
ulimwengu wa sasa pasipo kuwepo na vifaa bora vya mawasiliano dunia haito weza
kuwa ya kisasa kama inavyo hitajika hivyo kuwataka wanafunzi wa Shule hiyo
pamoja na Waalimu kuweza kutumia vifaa hivyo kwa makini ikiwa ni pamoja na
kutumika katika malengo mahususi.
“Niombe sana
vifaa hivi vitumike kwa malengo maalumu yatakayo weza kujenga kizazi kizuri
chenye faida kwa Taifa,sitegemei kusikia kuwa vifaa hivi vitatumika kufanya
mambo yatakayo bomoa maadili na malengo mahususi”.Alisema Byakanwa.
Byakanwa
ametaka uongozi wa shule hiyo kuanza kutumia kompyuta hizo kwa kutumia waalimu
waliopo shuleni hapo wenye uelewa wa kutumia vifaa hivyo,wakati wakisubiri waalimu
wa masomo hayo kupangwa kuja shuleni hapo.
Ameongeza
kuwa ofisi yake kwa kushirikiana na Afisa elimu watashughulikia upatikanaji wa
waalimu walio fuzu kufundisha mambo ya mawasiliano watakao tumika katika shule
hiyo kutoa elimu kwa wanafunzi na zoezi la kuwapata waaalimu hao halita zidi
miezi mitatu.
Aidha ametoa
agizo kwa shule zote za sekondari pamoja na bodi za shule kuhakikisha kuwa wanaandika majina ya watoto
walio fanya vizuri kwenye kuta na vibao
katika shule zao ili kuweza kuongeza chachu ya ufaulu kwa wanafunzi kushindania
kwa majina yao kubaki kumbukumbu.
Kwa upande
wake Mkurugenzi wa NMB Tanzania Bi.Ineke Bussemaker amesema kuwa Benki ya NMB inatambua umuhimu
wa elimu katika kumfanya Kijana wa sasa kuwa kijana mzuri kwa manufaa ya kesho kwa kumjengea
uwezo katika teknolojia ya mawasiliano.
Ameongeza
kuwa elimu inasaidia kuhakikisha kuwa taifa linaendelea kwa kupitia mchango wa
elimu hivyo kuwataka wanafunzi hao kuhakikisha kuwa wanatumia muda wao vizuri
ili kuweza kufikia malengo ya mmoja moja
na Taifa.